Jumamosi, 20 Agosti 2016

MWONGOZO WA KOZI YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU 2016/2017



ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY TANZANIA
ECHASE
SEMINARI YA MAVUNO ELAM
P.O.Box 69 Mkwajuni Mbeya. Tel 0762532121. Emai elamseminary@gmail.com



Kuwaandaa Watendakazi kwaajili ya Mavuno ya Nyakati za Mwisho.
LUKA 10:2

 KIHUNZI CHA KOZI

SEMISTA YA   SITA
IDARA:                                   Idara Ya  Theologia
MSIMBO WA KOZI:           ED T 606
 JINA LA KOZI :         UPAKO WA ROHO MTAKATIFU
 UKUBWA WA KOZI :       Krediti 3.

MHADHIRI: Rev. Erick .L. M
I.                  MAELEZO YA KOZI
Kozi hii ya Upako wa Roho Mtakatifu  Inapitia na kujadili kwa kina  Juu ya upako wa Roho Mtakatifu. Inachunguza, kuchambua na kuainisha jinsi Upako wa Roho Mtakatifu ulivyo na namna unavyotendakazi katika maisha ya Mwamini na viongozi na watendakazi wa kanisa. Aidha Kozi hii inachunguza kanuni mbalimbali za kupokea upako na jinsi na namna ya kufanya ili kutembea katika Upako wa Roho Mtakatifu. Kozi hii inaweka mkazo katika kuwapa changamoto waamini, Watendakazi na viongozi wa Kanisa   kutembea  na kufanya kazi ya huduma katika upako wa Roho Mtakatifu.


II.               MALENGO YA KOZI
Kozi hii  inalenga  kuwawezesha Wanafunzi kufanya kazi ya huduma katika upako wa Roho Mtakatifu.  Inalenga kuwapa hamasa viongozi, Watendakazi na Waamini  wote kwa ujumla kujihusisha katika Upako wa Roho Mtakatifu.
Baada ya kujifunza Kozi hii mwanafunzi ataweza, Kueleza dhana ya Upako wa Roho Mtakatifu, Kanuni za Upako wa Roho Matakatifuu, namna  Upako wa Roho Mtakatifu unavyotenda kazi, kweli kadhaa kuhusu Upako wa Roho Mtakatifu,  Jinsi ya kutunza Upako na namna ya kupokea upako  mara tatu. Baaada ya kujifunza Kozi hii mwanafunzi anatarajiwa kuanza kuishi, kutembea  kutenda na kufanya kazi ya Huduma kwa upako wa Roho Mtakatifu.



III.           MAUDHUI YA KOZI

MODULI YA KWANZA: UTANGULIZI WA KIHISTORIA NA KINABII JUU YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU.
1.     Dhana ya Upako wa Roho Mtakatifu
2.     Upako katika Agano la kale
a)     Asili ya neno Upako
b)    Asili ya neno Masihi

3.     Upako katika Agano Jipya
a)     Aleopho
b)    Chrio
c)     Charisma

MODULI YA PILI:  AILI, MAKUSUDI NA MATUMIZI YA UPAKO
A.   Asili ya Upako
B.   Kusudi la Upako
C.   Kazi ya Upako


MODULI YA TATU: KUTEMBEA KATIKA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU
A.   Namna ya kupokea Upako wa Roho Mtakatifu
B.   Kukua katika upako wa Roho Mtakatifu
C.   Kulinda upako Wa Roho Mtakatifu
MODULI YA NNE:     KUPOKEA UPAKO MARA TATU
  Utangulizi
A.   Upako wa aina tatu
1.     Upako wa Mkoma
2.     Upako wa kuhani
3.     Upako wa Kifalme.
B.    Mifano ya Upako mara tatu
C.   Upako uliogawanyika
D.   Hitimisho
IV.       MBINU ZA UFUNDISHAJI
Kozi hii ina jumla ya masaa 30 ya ufundishaji na masaa 15 ya semina na jumla ya masaa 45 ya ujifunzaji na ufundishaji.  Kozi itafundishwa kwa  kutumia mbinu na njia mbalimbali. Kozi itafundishwa kwa kutumia  mbinu   Shirikishi  ambapo mwanafunzi atakuwa mtendaji mkuu. Baadhi ya njia zitakazotumiwa ni  Mhadhara, onesho, Majadiliano,   Semina na uwasilishaji.

V.         TATHMINI  NA UPIMAJI
 Kozi hii itakuwa na Tathimini mbili, tathmini moja itakuwa ni ya  mhadhiri  ambapo  Mhadhiri  atawatathmini wanafunzi kupitia mazoezi na mtihani wa mwisho wa Semista. Tathmini ya pili itakuwa ni ya wanafunzi ambapo wanafunzi wataitathimini Kozi,  Mhadhiri  na mwenendo mzima wa ufundishaji na Ujifunzaji wa kozi. Kila mwanafunzi anatakiwa kushiriki kikamilifu katika kujifunza na kufuata maelekezo yanayotolewa  na mhadhiri wa Kozi.
Kozi hii itakuwa na mchanganuo ufuatao wa alama
·        Jaribio la 1 alama 10
·        Jaribio la 2 alama 10
·        Kazi ya kundi alama 5
·        Kazi ya binafsi alama 10
·        Mahudhurio alama 5
·        Jumla ya Tamrini alama 40
·        Mtihani wa Seminari alama 60
·        Jumla ya alama 100.





VI.                                      MAREJEO


Mahony R,1996, Kupokea Upako mara tatu, Fimbo ya mchungaji. Kilpaul, Chennai 600 010, T.N., INDIA.
Miller, R.M () Huduma yenye Nguvu: Uhudumu katika nguvu na upako wa Roho Mtakatifu. Springfield, MO, USA
 Parrish,F, R, () Upako wa Roho Mtakatifu: (2014) Matendo: Kilpaul, Chennai 600 010, T.N., INDIA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni