Jumamosi, 20 Agosti 2016

Mwongozo wa Kozi ya MISINGI YA IMANI



ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY TANZANIA
ECHASE
SEMINARI YA MAVUNO ELAM
P.O.Box 69 Mkwajuni Mbeya. Tel   0762532121.  Email. elamseminary@gmail.com

Kuwaandaa Watendakazi kwaajili ya Mavuno ya Nyakati za Mwisho.LUKA 10:2

MWONGOZO WA KOZI

SEMISTA YA   KWANZA.
IDARA:                                   Idara Ya   Theologia.
MSIMBO WA KOZI:           EDT 100
 JINA LA KOZI:                       Misingi ya Imani.
 UKUBWA WA KOZI:       Krediti 2.

I.         MAELEZO YA KOZI
Kozi hii inapitia na kutalii Misingi ya Imani ya Kikristo. Katika kozi hii mwanafunzi atajifunza misingi mbalimbali ya  imani ya Kikristo ambayo kwayo Ukristo umejengwa. Pia kozi hii ina utathmini Ubora wa Ukristo na upee wake ukilinganishwa na dini zingine zote. Kwa Kuwa misingi ya kitu chochote  ndiyo inayotathmini ubora wa kitu hicho, hivyo basi kozi hii inatoa changamoto kwa viongozi na watendakazi wa Kanisa katika kuifundisha misingi ya imani kwa waamini wao na kuitetea Imani ya Kikristo kwa uthabiti.  Misingi anuai ya imani Ya Kikristo itapitiwa na kujadiliwa kwa kina katika Kozi hii.


                                          
II.       MALENGO YA KOZI
Kozi hii inalenga kuwapa wanafunzi ujuzi stadi na Maarifa juu ya Misingi ya imani ya Kikristo. Pia inalenga kuweka tofauti bayana kati ya Imani ya Kikristo na imani ya dini zingine.Baada ya Kujifunza Kozi hii mwanafunzi atakuwa na uwezo wa, Kuainisha Misingi anuai ya Imani ya Kikristo, Kueleza upekee wa Imani ya kikristo, kuchambua na kuitathmini Imani ya Kikristo. Pia mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kufundisha juu ya Misingi ya Imani ya Kikristo  na kuelezea mpango wa Mungu kwa ulimwengu mzima.
III.     MAUDHUI YA KOZI.
MADA YA 1: UFAFANUZI WA ISTILAHI.
·        Dhana ya Msingi
·        Dhana ya Imani
·        Dhana ya Ukristo
·        Dhana ya misingi ya Imani
·        Sababu za kujifunza Misingi ya Imani.

MADA YA 2:  UWEPO WA MUNGU
·        Dhana ya uwepo wa Mungu
·        Njia ambazo Mungu ametumia kujidhihirisha
·        Tabia Za Mungu
·        Sifa za Mungu
·        Utatu wa Mungu.

MADA YA 3: BIBLIA NENO LA MUNGU LISILO NA MAKOSA.
·        Mamlaka iliyo kuu na ya mwisho katika imani, mafundisho na mwenendo wa Imani ya Kikristo.
·        Sababu za kuiamini Biblia kuwa Neno la Mungu.
·        Kazi ya maandiko Matakatifu.
MADA YA 4: ANGUKO LA MWANADAMU
·        Kuumbwa kwa Mwanadamu
·        Anguko la Mwanadamu
·        Matokeo ya Anguko la Mwanadamu
·        Hitaji la wokovu kwa Mwanadamu
·        Mbingu na Jehanamu
·        Kiyama ya wafu.

·        MADA YA 5: WOKOVU KWA NEEMA KWA NJIA YA IMANI
·        Dhana ya wokovu.
·        Dhana ya Neema
·        Damu ya Yesu ilitosha kwa ukombozi kamili.
·        Mifano ya Yesu Kristo katika Agano la kale
·        Maandalio ya wokovu.
MADA YA 6: KUHESABIWA HAKI KWA NJIA YA IMANI
·        Dhana ya haki
·        Haki ya Mungu dhidi ya mwenye dhambi
·        Upendo wa Mungu kwa mwenye Dhambi.
·        Kukutana kwa haki na Upendo wa Mungu dhidi ya mwenye dhambi.
MADA YA 7: KANISA KIUMBE HAI CHA KI-MUNGU DUNIANI
·        Dhana ya kanisa
·        Aina ya makanisa
·        Kazi kuu tatu za Kanisa.
·        Kusudi la kuwepo kwa Kanisa.
·        Maagizo makuu ya kanisa.
MADA YA 8: ROHO MTAKATIFU NI MUNGU.
·        Dhana ya Roho Mtakatifu.
·        Ushahidi wa  Roho Mtakatifu kuwa ni  Mungu.
·        Kazi za Roho Mtakatifu.
·        Ujazo wa Roho Mtakatifu.
·        Umuhimu wa Kunena kwa lugha mpya.



·        MADA YA 9 : YESU NI MUNGU
·        Ahadi ya kuzaliwa kwa masihi
·        Kuzaliwa kwake na Bikira
·        Ushahidi wa Yesu Kristo kuwa ni Mungu.
·        Yesu Kristo Mungu Kamili na Mwanadamu Kamili.

IV.       MBINU ZA UFUNDISHAJI
Kozi itafundishwa kwa  kutumia mbinu na njia mbalimbali. Kozi itafundishwa kwa kutumia  mbinu   Shirikishi  ambapo mwanafunzi atakuwa mtendaji mkuu. Baadhi ya njia zitakazotumiwa ni  Mhadhara, onesho, Majadiliano,   Semina na uwasilishaji.

V.         TATHMINI  NA UPIMAJI
 Kozi hii itakuwa na Tathimini mbili, tathmini moja itakuwa ni ya  mhadhili ambapo  Mhadhili  atawatathmini wanafunzi kupatia mazoezi na mtihani wa mwisho wa Semista. Tathmini ya pili itakuwa ni ya wanafunzi ambapo wanafunzi wataitathimini Kozi,  Mhadhili  na mwenendo mzima wa ufundishaji na Ujifunzaji wa kozi.
Kozi hii itakuwa na mchanganuo ufuatao wa alama
·        Jaribio la 1 alama 10
·        Jaribio la 2 alama 10
·        Kazi ya kundi alama 5
·        Kazi ya binafsi alama 10
·        Mahudhurio alama 5
·        Jumla ya Tamrini alama 40
·        Mtihani wa Seminari alama 60
·        Jumla ya alama 100.





VI.       MAREJEO
Marejeo  yataandaliwa na kutolewa na   Mhadhiri atakaefundisha Kozi hii.

MTAALA HUU UMEANDALIWA NA KURUGENZI YA MAADIKO NA MACHAPSHO
NOVEMBA 2015

………………………………………

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni