ELAM CHRISTIAN
HARVEST SEMINARY TANZANIA
ECHASE
SEMINARI
YA MAVUNO ELAM
P.O.Box 69 Mkwajuni Mbeya. Tel 0762532121.
Email. elamseminary@gmail.com

Kuwaandaa
Watendakazi kwaajili ya Mavuno ya Nyakati za Mwisho.
LUKA
10:2
JINA LA KOZI: KARAMA
ZA ROHO MTAKATIFU
MSIMBO WA KOZI: EDT 301
MHADHIRI: Rev.
ERICK L. (M. Div)
I.
MAELEZO
YA KOZI
Kozi
hii ya Karama za Roho Mtakatifu inachunguza,
kuchambua na kuainisha karama tisa (9) za
kiutendaji za Roho Mtakatifu kama zinavyoelezwa katika Maandiko Matakatifu
(Biblia). Inajadili namna Karama hizi zinavyotenda kazi na namna mwamini na kiongozi wa kanisa anavyoweza
kuhudumu katika Karama za Roho Mtakatifu. Kozi hii pia Kujadili umuhimu wa Karama za
Roho Mtakatifu katika kanisa katika karne zote
II.
MALENGO
YA KOZI
Kozi
hii inalenga kutazama zaidi Asili, utendajikazi na matumizi ya Karama za
Roho Mtakatifu kama vilivyofunuliwa na kuelezwa katika Maandiko Matakatifu, Kutoa msimamo wa ki-Biblia na ki-Theolojia juu ya utekelezaji na utendaji wa Karama. Kueleza sehemu zenye utata na mafundisho
yasiyo ya ki-Biblia kuhusu karama za Roho Mtakatifu.
Baada ya kujifunza Kozi
hii mwanafunzi aweze :-
v Kueleza
dhana ya Karama
v Kufafanua
dhana ya Karama za Roho Mtakatifu
v Kueleza
asili ya Karama Za Roho Mtakatifu
v Kujadili
Makusudi ya kutolewa kwa Karama za Roho
Mtakatifu
v Kuainisha
aina mbalimbali za Karama za Roho Mtakatifu
v Kuzigawa
karama za Roho Mtakatifu katika mafungu au makundi matatu
v Kujadili
kila karama namna inavyotenda kazi na namna mwamini anavyoweza kuhudumu katika
karama husika.
v Kujadili
nadharia za ukomo wa ishara na miujiza katika kanisa
v Kutathmini
utendajikazi wa ishara na maajabu katika
historia ya Kanisa tangu mwka 100 B.K hadi sasa.
III.
MAUDHUI
YA KOZI
MODULI YA KWANZA: ROHO
MTAKATIFU
i.
Dhana ya Roho Mtakatifu
ii.
Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu
iii.
Ubatizo wa Roho Mtakatifu
MODULI YA PILI: ROHO MTAKATIFU NA
MWAMINI
i.
Roho Mtakatifu humsaidia Mwamini
ii.
Kumpokea Roho Mtakatifu
iii.
Kunena/kusema kwa lugha
MODULI YA TATU: KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
i.
Dhana
ya Karama
ii.
Dhana ya Karama za Roho Mtakatifu
iii.
Asili ya Karama za Roho Mtakatifu
iv.
Madhumuni/ Makusudi ya kutolewa kwa
Karama za Roho Mtakatifu
v.
Umuhimu wa Karama za Roho Mtakatifu
katika Kanisa.
vi.
Nia yetu tunapohudumu katika Karama za
Roho Mtakatifu.
vii.
Aina za Karama za kiutendaji za roho
Mtakatifu
viii.
Makundi ya Karama za Roho Mtakatifu.
MODULI YA NNE: KARAMA ZA NDIMI/USEMI/UVUVIO
i.
Dhana ya Karama za ndimi
ii.
Karama
ya aina za Lugha
a. Dhana
ya aina za lugha
b. Namna
karama ya aina za Lugha inavyotendakazi
c. Madhumuni
ya Karama ya Aina za Lugha
d. Mwongozo
wa kimatumizi wa Karama ya Aina za Lugha
iii.
Karama
ya Tafsiri za Lugha
a. Dhana
ya Tafsiri za Lugha
b. Madhumuni
ya Karama ya Tafsiri za Lugha
c. Namna
Karama ya Tafsiri za Lugha inavyotendakazi
d. Masharti
ya Karama ya Tafsiri za Lugha
e. Mwongozo
wa kimatumizi wa Karama ya Tafsiri za Lugha
iv.
Karama
ya Unabii
a. Dhana
ya unabii
b. Tofauti
kati ya hudma ya nabii na Karama ya Unabii.
c. Kusudi
la Karama ya unabii
d. Vile
Karama ya Unabii isivyo
e. Mwongozo
wa kupima Unabii
f. Mwongozo
wa kimatumizi wa Karama ya Unabii
MODULI YA TANO: KARAMA ZA
UFUNUO
i.
Dhana ya Karama za Ufunuo
ii.
Kusudi la Karama za ufunuo
iii.
Aina ya Karama za Ufunuo
iv.
Karama ya Neno la Maarifa.
a. Fasili
ya Neno la Maarifa
b. Vile
Karama ya Neno la Maarifa isivyo.
c. Makusudi
ya Karama ya Neno la Maarifa
d. Jinsi Karama ya Neno la Maarifa invyotendakazi
e. Mwongozo
wa Kimatumizi/utendaji wa Karama ya Neno la Maarifa.
v.
Karama
ya Neno la Hekima
a. Fasili
ya Neno la Maarifa
b. Vile
Karama ya Neno la Hekima isivyo
c. Uhusiano
kati ya Neno la Hekima na Neno la Maarifa.
d. Madhumuni/Makusudi
ya Karama ya Neno la Hekima
e. Namna
Karama ya Neno la Hekima inavyotenda kazi
f. Mwongozo
wa kiutendaji wa Karama ya Neno la
Hekima
vi.
Kupambanua
roho.
a. Fasili
ya kupambanua roho
b. Vile
Karama hii isivyo
c. Madhumuni
ya Karama ya Kupambanua roho
d. Namna
Karama ya Kupambanua roho inavyotenda
kazi.
e. Mwongozo
wa kiutendaji wa Karama ya Kupambanua roho.
MODULI
YA SITA: KARAMA ZA NGUVU/ UWEZO
i.
Fasili ya Karama za nguvu
ii.
Aina ya Karama za Nguvu
iii.
Madhumuni ya Karama za Nguvu.
iv.
Karama
ya Imani
a. Fasili
ya Karama ya Imani
b. Madhumuni
ya Karama ya Imani
c. Uhusiano
kati ya Karama ya Imani na Karama nyingine za Nguvu
d. Namna
Karama ya Imani inavyotenda kazi
e. Mwongozo
wa Kiutendaji wa Karama ya Imani
v.
Karama
za Uponyaji
a. Fasili
ya Karama za Uponyaji
b. Madhumuni
ya Karama za Uponyaji
c. Namna
Karama za Uponyaji inavyotenda kazi.
d. Mwongozo
wa kiutendaji wa Karama za Uponyaji.
vi.
Karama
ya Matendo ya Miujiza
a. Fasili
ya Mtendo ya Miujiza
b. Madhumuni
ya Karama ya Matendo ya Miujiza
c. Namna
Karama ya Matendo ya Miujiza inavyotenda kazi
d. Mwongozo
wa Kiutendaji wa Karama ya Matendo ya
Miujiza.
MODULI YA SABA: ISHARA NA MAAJABU SIKU HIZI
i.
Usuli
ii.
Nadharia za Ukomo wa Ishara na Miujiza
iii.
Mapungufu ya Nadharia za Ukomo
iv.
Mawazo ya Wana-Injili wasiokubali
mabadiliko.
MODULI YA NANE: ISHARA NA MAAJABU KATIKA HISTORIA YA
KANISA
i.
Fasili ya Ishara na Maajabu
ii.
Kipindi cha Kale Miaka ya 100-600. B.K
iii.
Kipindi cha Kati Miaka ya 600 - 1500
B.K
iv.
Wakati wa Matengenezo ya Kanisa Miaka ya
1500 - 2000
Wakati wa sasa.
IV.
MBINU ZA UFUNDISHAJI
Kozi
hii ina masaa 30 ya Mihadhara na Masaa 15 ya Semina, jumla
ina masaa 45 ya ufundishaji. Kozi
itafundishwa kwa kutumia mbinu na njia
mbalimbali. Kozi itafundishwa kwa kutumia
mbinu Shirikishi ambapo mwanafunzi atakuwa mtendaji mkuu.
Baadhi ya njia zitakazotumiwa ni
Mhadhara, onesho, Majadiliano,
Semina na uwasilishaji.
V.
TATHMINI NA UPIMAJI
Kozi
hii itakuwa na Tathimini mbili, tathmini moja itakuwa ni ya mhadhili ambapo Mhadhili atawatathmini wanafunzi kupitia mazoezi na
mtihani wa mwisho wa Semista. Tathmini ya pili itakuwa ni ya wanafunzi ambapo
wanafunzi wataitathimini Kozi,
Mhadhili na mwenendo mzima wa
ufundishaji na Ujifunzaji wa kozi.
Kozi hii itakuwa na mchanganuo ufuatao
wa alama
·
Jaribio la 1 alama 10
·
Jaribio la 2 alama 10
·
Kazi ya kundi alama 5
·
Kazi ya binafsi alama 10
·
Mahudhurio alama 5
·
Jumla
ya Tamrini alama 40
·
Mtihani wa Seminari alama 60
·
Jumla
ya alama 100.
MAREJEO
Gill,A,
L (1995) Maisha ya Miujiza- ISOM Muhula wa kwanza. USA
Peter,
W (1985) Your Spiritual gift can help your church grow. Kent Cox al Wyman
Rawland,G
(1996)Kupokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu na Karama zake: Fimbo ya
Mchungaji.Indira Printers.New Delh 110020.
Thomas,
A.P (1992) Karama za Rohoni: Jinsi Pentekoste inavyofanya kazi na kukaribia
watu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni