Jumamosi, 20 Agosti 2016

mwongozo wa Kozi ya BIBLIOLOGIA



ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY TANZANIA
ECHASE
SEMINARI YA MAVUNO ELAM
P.O.Box 69 Mkwajuni Mbeya. Tel 0762532121. Emai elamseminary@gmail.com

Kuwaandaa Watendakazi kwaajili ya Mavuno ya Nyakati za Mwisho.LUKA 10:2
MWONGOZO WA KOZI

SEMISTA YA KWANZA.
IDARA:                                   Idara Ya  Theologia
MSIMBO WA KOZI:           EDT 105
 JINA LA KOZI:                    Bibliolojia
 UKUBWA WA KOZI :       Krediti 3.

I.                  MAELEZO YA KOZI
Kozi hii ya Bibliolojia inachunguza historia ya Biblia na kuthibitisha ukweli wa Biblia kuwa Neno la Mungu.Katika kozi hii mwanafunzi atajifunza stadi na maarifa mbalimbali yahusuyo elimu ya Biblia. Mwanafunzi atajifunza upekee Wa Biblia na Ubora wake ikilinganishwa na vitabu vingine vya dini, nyingine, Sayansi na Falsafa.
Katika Kozi hi mwanafunzi atajifunza hatua mbalimbali Biblia ilizopitia  tangu kuandikwa kwake hadi kuenea kwake ulimwenguni kote. Pia  Kozi hii inatazama jinsi Biblia ilivyopambana na maadui zake na kuwashinda.  Kozi hii ni kozi ya msingi katika Kozi zote za Theologia  ya Kikristo. Inasimama kama daraja la kozi zingine za Theologia.  

II.               MALENGO YA KOZI.
Kozi hii inalenga kumjengea mwanafunzi msingi wa kitheologia ya Kikristo ambayo kiini chake ni Biblia Takatifu.Baada ya kujifunza Kozi hii mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kueleza jinsi Biblia ilivyoandikwa,lugha za Biblia, Jinsi Biblia ilivyopambana na Maadui zake na kuwashinda kabisa. Jinsi vitabu vya Biblia vilivyokusanywa na kuwekwa pamoja kuwa  kitabu kimoja.  Pia mwanafunzi ataweza kutoa ushahidi wa Biblia kuwa Neno la Mungu na kuweza kueleza jinsi  Mungu alivyohusika katika uandishi wa Biblia, kuhifadhiwa kwake na jinsi Mungu anavyohusika sasa kwa wasomaji wa Biblia. Pia mwanafunzi ataweza kueleza Mpango wa Mungu kwa ulimwengu zima kama Biblia inavyofundisha. Baada ya kujifunza kozi hii mwanafunzi anatarajiwa kuwa shahidi mwaminifu wa imani Ya ki- kristona kutetea ukweli wa Ki- Mungu siku zote za maisha yake.

III.           MAUDHUI YA   KOZI.
MADA  YA 1. USULI WA BIBLIA.
·        Asili ya Neno-Biblia
·        Maana ya Biblia.
·        Kiini cha Biblia
·        Ujumbe wa Biblia
·        Lugha za Biblia
·        Umoja wa Biblia
·        Nyakati za kuandikwa kwa Biblia
·        Tafsiri za Biblia za Zamani sana
·        Nakala za Biblia za zamani zilizopo leo.
·        Sababu za kujifunza Biblia



MADA YA  2. USHAHIDI WA BIBLIA KUWA NENO LA MUNGU.
·        Uwezo wa Biblia kubadili maisha ya watu
·        Unabii uliotimizwa na unaoendelea kutimizwa
·        Kujibiwa kwa maombi
·        Ushahidi wa uchimbuaji.
·        Umoja waBiblia.

MADA YA 3: KANUNI YA BIBLIA
·        Dhana  ya Kanuni
·        Maana ya Kanuni ya Biblia
·        Sababu za kuwa na Kanuni ya Biblia.
·        Kanuni za Biblia.
·        Vitabu vya Apokrifa.

MADA YA 4: KUENEZWA KWA BIBLIA ULIMWENGUNI KOTE.
·        Peter Waldo
·        John Wyklif
·        Wiliam Tyndale.
·        Kutafsiriwa kwa Biblia Duniani kote.

I.            MBINU ZA UFUNDISHAJI
Kozi itafundishwa kwa  kutumia mbinu na njia mbalimbali. Kozi itafundishwa kwa kutumia  mbinu   Shirikishi  ambapo mwanafunzi atakuwa mtendaji mkuu. Baadhi ya njia zitakazotumiwa ni  Mhadhara, onesho, Majadiliano,   Semina na uwasilishaji.



II.          TATHMINI  NA UPIMAJI
 Kozi hii itakuwa na Tathimini mbili, tathmini moja itakuwa ni ya  mhadhili ambapo  Mhadhili  atawatathmini wanafunzi kupatia mazoezi na mtihani wa mwisho wa Semista. Tathmini ya pili itakuwa ni ya wanafunzi ambapo wanafunzi wataitathimini Kozi,  Mhadhili  na mwenendo mzima wa ufundishaji na Ujifunzaji wa kozi.
Kozi hii itakuwa na mchanganuo ufuatao wa alama
·        Jaribio la 1 alama 10
·        Jaribio la 2 alama 10
·        Kazi ya kundi alama 5
·        Kazi ya binafsi alama 10
·        Mahudhurio alama 5
·        Jumla ya Tamrini alama 40
·        Mtihani wa Seminari alama 60
·        Jumla ya alama 100.

III.       MAREJEO
Marejeo  yataandaliwa na kutolewa na   Mhadhiri atakaefundisha Kozi hii.

MTAALA HUU UMEANDALIWA NA KURUGENZI YA MAADIKO NA MACHAPSHO
NOVEMBA 2015

………………………………………

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni