ELAM
CHRISTIAN HARVEST SEMINARY TANZANIA
ECHASE
SEMINARI
YA MAVUNO ELAM
Kuwaandaa Watendakazi kwaajili ya Mavuno ya Nyakati za Mwisho.
LUKA 10:2
KIHUNZI CHA
KOZI
SEMISTA YA SITA
IDARA: Idara
Ya Theologia
MSIMBO WA KOZI: ED T 606
JINA LA KOZI : UPAKO WA ROHO MTAKATIFU
UKUBWA WA KOZI : Krediti 3.
MHADHIRI:
Rev. Erick .L. M
I.
MAELEZO
YA KOZI
Kozi
hii ya Upako wa Roho Mtakatifu Inapitia
na kujadili kwa kina Juu ya upako wa
Roho Mtakatifu. Inachunguza, kuchambua na kuainisha jinsi Upako wa Roho
Mtakatifu ulivyo na namna unavyotendakazi katika maisha ya Mwamini na viongozi
na watendakazi wa kanisa. Aidha Kozi hii inachunguza kanuni mbalimbali za
kupokea upako na jinsi na namna ya kufanya ili kutembea katika Upako wa Roho
Mtakatifu. Kozi hii inaweka mkazo katika kuwapa changamoto waamini, Watendakazi
na viongozi wa Kanisa kutembea na kufanya kazi ya huduma katika upako wa
Roho Mtakatifu.
II.
MALENGO
YA KOZI
Kozi hii inalenga kuwawezesha Wanafunzi kufanya kazi ya huduma
katika upako wa Roho Mtakatifu. Inalenga
kuwapa hamasa viongozi, Watendakazi na Waamini
wote kwa ujumla kujihusisha katika Upako wa Roho Mtakatifu.
Baada ya kujifunza Kozi hii mwanafunzi
ataweza, Kueleza dhana ya Upako wa Roho Mtakatifu, Kanuni za Upako wa Roho
Matakatifuu, namna Upako wa Roho
Mtakatifu unavyotenda kazi, kweli kadhaa kuhusu Upako wa Roho Mtakatifu, Jinsi ya kutunza Upako na namna ya kupokea
upako mara tatu. Baaada ya kujifunza
Kozi hii mwanafunzi anatarajiwa kuanza kuishi, kutembea kutenda na kufanya kazi ya Huduma kwa upako
wa Roho Mtakatifu.
III.
MAUDHUI
YA KOZI
MODULI
YA KWANZA: UTANGULIZI WA KIHISTORIA NA KINABII JUU YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU.
1. Dhana
ya Upako wa Roho Mtakatifu
2. Upako
katika Agano la kale
a) Asili
ya neno Upako
b) Asili
ya neno Masihi
3. Upako
katika Agano Jipya
a) Aleopho
b) Chrio
c) Charisma
MODULI
YA PILI: AILI, MAKUSUDI NA MATUMIZI YA
UPAKO
A.
Asili
ya Upako
B.
Kusudi
la Upako
C.
Kazi
ya Upako
MODULI
YA TATU: KUTEMBEA KATIKA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU
A.
Namna ya kupokea Upako wa Roho Mtakatifu
B.
Kukua katika upako wa Roho Mtakatifu
C.
Kulinda upako Wa Roho Mtakatifu
MODULI
YA NNE: KUPOKEA UPAKO MARA TATU
Utangulizi
A.
Upako wa aina tatu
1. Upako
wa Mkoma
2. Upako
wa kuhani
3. Upako
wa Kifalme.
B.
Mifano ya Upako mara tatu
C.
Upako uliogawanyika
D.
Hitimisho
IV.
MBINU ZA UFUNDISHAJI
Kozi
hii ina jumla ya masaa 30 ya ufundishaji na masaa 15 ya semina na jumla ya
masaa 45 ya ujifunzaji na ufundishaji. Kozi
itafundishwa kwa kutumia mbinu na njia
mbalimbali. Kozi itafundishwa kwa kutumia
mbinu Shirikishi ambapo mwanafunzi atakuwa mtendaji mkuu.
Baadhi ya njia zitakazotumiwa ni
Mhadhara, onesho, Majadiliano,
Semina na uwasilishaji.
V.
TATHMINI NA UPIMAJI
Kozi hii itakuwa na
Tathimini mbili, tathmini moja itakuwa ni ya mhadhiri ambapo Mhadhiri atawatathmini wanafunzi kupitia mazoezi na
mtihani wa mwisho wa Semista. Tathmini ya pili itakuwa ni ya wanafunzi ambapo
wanafunzi wataitathimini Kozi, Mhadhiri na mwenendo mzima wa ufundishaji na
Ujifunzaji wa kozi. Kila mwanafunzi anatakiwa kushiriki kikamilifu katika
kujifunza na kufuata maelekezo yanayotolewa
na mhadhiri wa Kozi.
Kozi
hii itakuwa na mchanganuo ufuatao wa alama
·
Jaribio la 1 alama 10
·
Jaribio la 2 alama 10
·
Kazi ya kundi alama 5
·
Kazi ya binafsi alama 10
·
Mahudhurio alama 5
·
Jumla ya Tamrini alama 40
·
Mtihani wa Seminari alama 60
·
Jumla ya alama 100.
VI. MAREJEO
Mahony R,1996, Kupokea Upako mara tatu, Fimbo ya
mchungaji. Kilpaul, Chennai 600 010, T.N., INDIA.
Miller, R.M () Huduma yenye Nguvu:
Uhudumu katika nguvu na upako wa Roho Mtakatifu. Springfield, MO, USA
Parrish,F, R,
() Upako
wa Roho Mtakatifu: (2014) Matendo: Kilpaul, Chennai 600 010, T.N., INDIA.