ELA
M CHRISTIAN HARVEST SEMINARY NI
CHUO cha Biblia cha kimishenari chenye msingi wa
Kipentekoste kinachotoa mafunzo katika
kuwaandaa Watendakazi na viongozi wa
Kanisa. Kwaajili ya Mavuno ya nyakati za
mwisho. Chuo hiki kinapokea wanafunzi
toka madhehebu yote
ya Kikristo
Tazama
ainisho la imani hapo chini
MAELEZO YA IMANI
33.0 AINISHO LA
MAELEZO YA IMANI
i.
Wokovu,
Tunaamini
kwamba wokovu upo duniani na kwamba baada ya kufa, hakuna kuokoka, tunaokoka
tukiwa duniani na si mbinguni.
ii.
Uwepo
wa Mungu mmoja tu aliye wa kweli, Tunaamini kwamba kuna
Mungu wa kweli mmoja tu Mungu mmoja aliyejidhihirisha katika nafsi tatu ambazo
ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
iii.
Biblia
Takatifu, Tunaamini kwamba Biblia ni neno la Mungu
lililovuviwa lisilo na makosa na ni ndio mamlaka ya mwisho na iliyokuu katika
maisha ya mwamini.
iv.
Anguko
la mwanadamu, Tunaamini kwamba mwanadamu alianguka
dhambini na dhambi inamtenga mbali na Mungu na hivyo anamhitaji mwokozi Yesu
Kristo.
v.
Wokovu
kwa njia ya neema.Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani pekee.
vi.
Ukombozi
kutoka dhambini kupitia kifo cha kidhabihu cha Yesu Kristo.
Tunaamini kwamba Mungu alifanyika mwili na kufa msalabani kama fidia au dhabihu
ya dhambi, na kwa njia hii mwanadamu anaweza kupatanishwa na Mungu tena.
vii.
Kanisa
moja tu ulimwenguni lililo mwili wa Kristo linalowaunganisha ndani yake waamini
wote wa kweli. Tunaamini kwamba Kanisa ni kiumbe hai
ambacho Mungu anakitumia kuufikia ulimwengu wote.
viii.
Uwepo
wa huduma tano za uongozi. Tunaamini kwamba Yesu Krisot
alitoa huduma tano za uongozi ambazo ni mitume, manabii, wainjilisti,
wachungaji na waalimu kwa kusudi la kuwaandaa watakatifu kwaajili ya huduma.
Huduma hizi zote zipo ndani ya kanisa
hata sasa. Hakuna huduma iliyokuwa ya muda tu bali zote zinatenda kazi hata
sasa.
ix.
Ufufuo
wa wafu, Tunaamini kuwa kuna maisha mengine baada ya kufa,
Kufa ni njia tu ya kuingia katika maisha mapya ya milele, na hivyo kutakuwa na
ufufuo wa wafu wote watakatifu
wataurithi uzima wa milele na waovu watatupwa katika ziwa la moto.
x.
Tumaini
la Baraka. Tunaamini
kwamba Yesu Kristo atarudi mara ya pili kulichukua kanisa yaani watakatifu na
kwenda nao mbinguni.
xi.
Uwepo
wa jehanamu. Tunaamini hukumu ya waovu na mwisho
wao ambao ni kutupwa katika ziwa la moto.
xii.
Uwepo
wa miujiza. Tunaamini kwamba miujiza ipo mpaka sasa ndani ya
kanisa na kwamba haikuwa kwaajili ya kipindi fulani tu cha kanisa, bali ni kwa
vizazi vyote mpaka Bwana Yesu atakaporudi.
xiii.
Maisha
matakatifu. Tunaamini
kwamba maisha matakatifu ndio msingi wa
ukristo. Bila kuishi maisha matakatifu hakuna ukristo.
xiv.
Ukuhani
wa waamini wote. Tunaamini kwamba kila mwamini wa kweli ni
kuhani, anaowajibu wa kumwendea Mungu na kusimama katika huduma. Mungu anataka kila mwamini amtolee dhabihu za
maombi, sifa na shukrani na kuzitangaza fadhili zake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni