Jumapili, 12 Machi 2017

DIPLOMA YA THEOLOJIA KWA NJIA YA INTANETI



ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY
ECHASE
SEMINARI YA MAVUNO ELAM
P.O.BOX 69 MKWAJUNI   SONGWE
Tel.   0762532121. Email.  elamseminary@gmail.com

Kuwaandaa Watendakazi kwaajili ya Mavuno ya Nyakati za Mwisho.
LUKA 10:2
DIPLOMA YA BIBLIA NA THEOLOJIA KWA NJIA YA INTANETI
Uongozi wa Chuo cha Biblia cha Elam    Christian Harvest Seminary unapenda kuwa tangazia umma wote   wanaopenda kujiendeleza katika Elimu ya Mambo ya Mungu (Theolojia)  kuwa imeanzisha program ya Mafunzo ya Biblia na Theolojia kwa njia ya Mtandao (Intaneti).
Tunatoa DIPLOMA YA BIBLIA NA  THEOLOJIA kwa njia ya Mtandao
Huna haja ya kuacha kazi yako na familia yako na kwenda chuoni kwa muda mrefu, Waweza kusoma ukiwa unaendelea na kazi yako na kufikia maono yako au ngazi unayotaka.
Diploma ya Biblia na Theolojia ina jumla ya masomo/kozi arobaini na mbili (42 ) zenye jumla ya krediti tisini  (90)
Mwanafunzi aweza kusoma kuazia kozi moja hado kozi tatu kwa mwezi. Mwanafunzi atatumiwa masomo na mitihani kwenye emaili yake na baada ya kujifunza na kufanya mitihani mwanafunzi atarudisha mitihani kupitia emaili ya chuo liyoko hapo juu.
GHARAMA ZA MASOMO
Chuo chetu kinatoa mafunzo kwa gharama nafuu kabisa inayomwezesha kila mtu kumudu.  Gharama zetu hulipwa kwa kila kozi.
·        Ada ya usajiri ni Tsh. 11,000/=
·        Ada ya kozi ni  Tsh. 15,000/=
·        Mwanafunzi aweza kulipa ada ya muhula mzima au ada ya kila kozi atakayosoma kwa muda husika.





LUGHA YA MAFUNZO
Masomo yanafundishwa kwa lugha mbili  Kiswahili na Kiingereza. Mwanafunzi atachagua lugha atakayotumua katika masomo yake.

Baada ya Mwanafunzi kufuzu kozi zote 42 atatunukiwa Diploma  ya Biblia na Theolojia.
Watu wote mnakaribishwa kujiunga na chuo hiki ili muweze kuandaliwa kwaajili ya mavuno ya Kiroho.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba za simu za hapo juu au kwa barua pepe ya hapo juu.
Wako katika Mavuno


Rev. G J Kagussa
Naibu Makamu Mkurugenzi Mkuu Taaluma.
ELAM CHRISITAN HARVEST SEMINARY






ORODHA YA KOZI NGAZI YA   STASHAHADA (DIPLOMA)
Programu ya Biblia na Theologia inalenga kuwaandaa watendakazi na viongozi wa kanisa wenye kujaa  upako wa Roho mtakatifu na wenye taaluma ya kutosha katika uwanja wa theologia, huduma za kanisa na sanaa. Pia inalenga kuwapa stadi na ujuzi na kuwajengea uwezo wa kumtumikia Mungu katika wito wao kwa ufanisi mkubwa. Baada ya mafunzo haya viongozi hawa watakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utumishi wao na kuweza kumzalia Mungu matunda yanayodumu. Pia wataweza kufanya shughuli za uongozi na kutumia raslimali mbalimbali katika kuujenga ufalme wa Mungu. Pia programu hii inalenga kuwandaa wanafunzi   kitaaluma ili wawe na uwezo mpana wa kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika fani mbalimbali za elimu ya ki-Mungu.
Programu hii inajumla ya krediti 90  na  itachukua miaka  mitatu ya  ya mafunzo darasani na nje ya darasa
Baadaya kuhitimu mafunzo mwanafunzi ataweza kufanya huduma mbalimbali kutegemeana na wito  wa Mungu au huduma iliyomo ndani yake.
ORODHA YA KOZI NGAZI YA   STASHAHADA (DIPLOMA)
Mwaka Wa Kwanza
Semista ya Kwanza
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDB 100
Uchunguzi Wa Agano la Kale
3
EDB 101
Uchunguzi wa Agano Jipya
3
ED T 100
Misingi ya Imani
2
EDM 100
Sifa na ibada
1
EDT 105
Bibliolojia
2
EDB 103
Mbinu za Kujifunza Biblia
2
EDA 100
Stadi za Mawasiliano na mbinu za Usomaji
2

Semista ya Pili
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDT 200
Kuisikia sauti ya Mungu
1
EDT201
Maisha ya Kikristo
2
EDT 202
Kanuni za kufasiri Maandiko
3
EDT 203
Kanisa
2
EDM 200
Huduma ya Ukombozi na uponyaji
2
EDM 201
Mbinu  za kufanya Uinjilisti
2
EDM 202
Homiletiksi
2
EDM  203
Mazoezi ya Vitendo I
1

Mwaka Wa Pili
Semista ya tatu
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDT 300
Historia ya Kanisa
2
EDL 300
Maandalio ya Uongozi .I
2
EDM 300
Vita vya Kiroho
2
EDC 300
Mbinu za Kupanda Makanisa
3
EDT 303
Wanawake katika Huduma
2
EDT 301
Karama Za Roho Mtakatifu
2
EDB  300
Danieli na Ufunuo wa Yohana
2

Semista ya nne
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDT 400
Agano la Mungu
2
EDP400
Saikolojia ya Biblia
2
EDT 400
Mahusiano ya Kikristo
2
EDC 400
Mbinu za Mazidisho ya Kiroho
3
EDB 400
Waebrania
2
EDT 405
Theolojia I
2
EDT  406
 Maandalio ya uongozi II
2
Mwaka wa Tatu
Semista ya Tano
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDL 500
Kanuni za Uongozi wa Kiroho
2
EDM 500
Theolojia ya Utendaji
2
EDM 501
Huduma ya Masaidiano
1
EDT 500
Ndoa na Familia ya Kikristo
3
EDT 505
Utafiti wa ki-Theolojia
2
EDT 502
Theolojia II
2
EDA 500
Ujasiliamali
2
EDL 502
Mazoezi ya Vitendo II
1
Semista  ya Sita
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDT 604
Dini zaUlimwengu
2
EDT 600
Huduma tano za Uongozi
1
EDP 600
Ushauri wa Kichungaji
3
EDT 601
Theolojia ya Kichungaji
2
EDL 600
Kuongoza kwa Kusudi
1
 EDA 600
Sayansi ya Jamii
1
EDM 600
Mbinu za Ufundishaji
2
EDT 602
Maadili ya Kichnungaji
2
EDT 606
Kupokea Upako wa Roho Mtakatifu
1