Alhamisi, 9 Mei 2019
Jumamosi, 9 Machi 2019
UTEUZI WA MKURUGENZI ELIMU MASAFA
Bwana Yesu apewe sifa
Napenda kuchukua nafasi hii
kumtambulisha kwenu wanafunzi wote MKURUGENZI WA ELIMU MASAFA wa
Elam Christian Harvest Seminary Tanzania
Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Elam
Christian Harvest Seminary imemteua Ndugu
Rev.
Respister Y. Bitumbe
kuwa Mkurugenzi wa Elimu Masafa (Director of Distance Learning System)
Majukumu yake Kama Mkurugenzi wa Elimu
Masafa ni kusimamia mafunzo kwa njia ya
Mtandao na Posta, pia kusimamia vituo vyote vya Mobile Training.
Hivyo basi wanafunzi wote wanaosoma kwa
njia ya mtandao na posta watasimamiwa
na mkurugenzi huyo na mawasiliano yote yatafanyika kwa mkurugenzi huyo
Mawasiliano yote kuhusu masomo na mitihani
yatafanyika kwake kwa simu namba
0782-471-320 au 0757887467
Pia waratibu wote wa vituo vya mafunzo
ya Mobile mnapaswa kuwasilisha taarifa za maendeleo ya vituo kwake.
Kumbuka kutaja namba yako ya usajiri,
majina yako kamili na program ya masomo
unayosoma.
Nawatakieni masomo mema
Mungu awabariki sana
Wenu katika Elimu ya Kikristo
Rev. S.A Mlekia
NAIBU
MAKAMU MKURUGENZI MKUU MIPANGO FEDHA NA UTAWALA
Jumapili, 13 Januari 2019
MAONO- UFUNGUO WA KUFAULU
Sura Ya 2
MAONO – UFUNGUO WA KUFAULU
COMPLIED BY Rev.Dr. EricK L Mponzi
(ThD) ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY TANZANIA
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU SIMU 07625332121
Dibaji
Sasa tumefika mahali muhimu katika
kujifunza juu ya kanuni za kufaulu. Tumeelezea na kuchunguza sehemu muhimu ya
wakati wetu uliopita na tuko tayari kuanza kutwaa wakati ujao na kuufanya uzae
mavuno ambayo Mungu anapenda.
A.
ANZA
KWA MAONO
Chunguza mchoro kwenye ukurasa huu. Ni
mshale unaoelekea mbele. Unaelekea upande wa wakati ujao.
Naita mshale huu “njia ya kufaulu” kwa sababu hizi ni hatua ambazo
kwazo, kiongozi Mkristo atatumia kufanikisha mapenzi na matakwa ya Mungu.
Mafanikio yote, malengo yote, taratibu zote – kila kitu anachotaka Mungu
ukifanye – ni laazima kianze pale mshale unapoanzia katika mchoro ule. Ni
lazima kianze na MAONO.
1.
Bila
Maono
Ili kuweza kuelewa vizuri maana niliyo
nayo ninapozungumza juu ya maono, kuna haja ya kujadili nini kinachotokea pasipokuwa
na maono. Mit 29:18 inafahamika vyema sana katika jamii ya wainjilisti : “Pasipo maono, watu huacha kujizuia
[watu huangamia]…”
Kitu kimoja kwa ujumla hakijafahamika juu ya mstari ule. Maono anayozumgumzia mwandishi wa
Mithali sio maono tu ya kuwaleta watu kwa Yesu. Sina ugomvi na matumizi hayo.
Lakini mwandishi wa Mithali anazungumzia juu ya maono ya kinabii.
(Katika Kiebrania neno hilo, “maono” ni neno “chazown” lililomaanisha “ufunuo” au “usia” – yaani, maono). Pasipo
na maono ya kinabii watu huangamia.
(Huacha Kujizuia). Tafsiri moja ninayoipenda imasema,
“Pasipo maono watu hukaa bila uangalifu,” yaa wasio na sheria na wasiozuiwa.
Wanaishi aina ya maisha yasiyokuwa na kusudi. Hivi ndivyo inavyotokea “mahali
pasipo na maono ya kinabii.”
Kwa mfano: Kwa miaka mingi nchi yangu
mwenyewe imepungukiwa na maono na kusudi. Taifa hili limekuwa kama meli
isiyokuwa na usukani na matokeo yake, tunakaa ovyo ovyo. Tunachukuliwa bila
mwelekeo maalum kupitia kwenye miamba hatari kando kando ya bahari.
Nilipokuwa mtoto, kulikuwepo na hisia ya
maono tuliyoshirikishwa katika shule yetu, ufahamu wa mlengo wa kibinafsi na kitaifa,
ufahamu wa kusudi. Leo tunapozungumza juu ya kuwagawia vijana aina hiyo ya
maono, wengi katika mamlaka kwenye taasisi ya elimu hutushtaki kwa kuwa wa dini
sana tusio na akili.
Lakini wakati nilipokuwa mdogo
tuliwafundisha watoto wetu aina ya mlengo na kusudi. Tuliisalimu bendera kwa
ufahari kila siku, tuliwaheshimu na kuwajali waanzilishi wa taifa, na
tulitambua kuwa sisi ni taifa lililozaliwa kuwa huru kwa mataifa mengine.
Maneno kwenye Sanamu yetu ya Uhuru yanasomeka “Nitwike uchovu wako, maskini
wako, msongamano wa watu wako wanaotamani kupumua kwa uhuru. …”.
Haikupita miaka mingi tangu tulipoanza
kufanya kama watu walioamini kuwa nchi
hii ilikuwa ni bandari ya uhuru. Sasa, tunakaa ovyo ovyo.
2.
Haja
Ya Kuwa Maono Dhahiri.
Sisi
ambao ni wahubiri mara kwa mara tunakuwa na mawazo mengi ambayo hayajapangiliwa
vizuri. Tunatoka katika malezi ya kitheologia ambayo si dhahiri. Tunajieleza
kwa maneno yenye maana isiyo dhahiri au mafumbo yenye ufafanuzi mpana, maana na
maelezo ambayo si wazi.
Mtu
fulani akituuliza ni nini lengo letu katika maisha, sisi husema, “Lengo langu
ni kumtukuza Mungu.” Je, ni kweli kuwa hili ni jibu la kiroho? Je, ni kweli
kuwa ni la ajabu? Ni wangapi wenu mmeng’amua kuwa ni maneno yenye maana hafifu
(nyuzinyuzi, isiyo wazi), hasa kwa mtu wa kawaida kule barabarani?
Jibu
la mtu wa wastani anayetembea huko barabarani litakuwa, “Ni nini anachozungumza
huyo mpumbavu wa dini?”
Kama ningaliwauliza ninyi wasomaji
kufafanua “kumtukuza Mungu”, kuna maana gani? Bila shaka ningalipata majibu
mengi kulingana na idadi ya wasomaji. Hakuna uwazi wa maelezo tukitumia maneno
kama hayo.
a.
Je!
Yaweza Kuelezeka? Ngoja niulize hapa: Wewe unadhani maono
yasiyowezekana kuwaelezea wengine yataweza kufaulu?
Kufanya kazi na kompyuta kumenifundisha
kuwa nahitaji kusafisha chumba cha stoo ya akili ya mawazo yangu. Kwa
kutokukijali, kimejaa vumbi na utando wa buibui.
Wakati uliopita sikuzumgumza kwa uwazi.
Nilitumia maneno yaliyosika kama ya kiroho lakini mimi mwenyewe pamoja na
wengine hatukuyaelewa kabisa. Hii ni kawaida kwa watu wengi wa dini.
Tunazungumza kwa namna ambayo watu wengine hawawezi hata kuelewa.
Kutimiza wito wako, ni lazima kwanza
ufafanue maono yako yawe dhahiri ukitumia maneno ya kueleweka, badala ya
kutumia changanyiko la maneno ya dini yasiyokuwa dhahiri. Ni lazima uanze na
maono yaliyo dhahiri na yaliyofafanuliwa.
b.
Fahamu
Kusudi la Mungu. Ni sawa kwa maisha yako na kwa huduma yako
pia. Sehemu ya mbele ya mshale kwenye mchoro wangu hapo juu ni maono. Kama huna
maono yaliyofafanuliwa kwa uwazi utakabiliana na maisha bila kusudi hata kama
wengine watafikiri kuwa wewe ni mtu mashuhuri.
Utapeperushwa na kila
upepo kwa sababu hutakuwa na dira, hakuna ramani ya kuendea. Utakuwa kama Banyani ambaye anajiona kama
jani la masika, lililotupwa juu ya ziwa la uzima, likielea ovyo ovyo kila
mahali mawimbi yanakolipeleka. Wakristo wengi huishi maisha yao kwa namna hiyo.
Hawawezi kutawala zile sehemu za maisha yao ambazo Mungu ameweka katika uwezo
wao.
Lakini Mungu hakupanga kwa namna hiyo. Anatamani kwamba tujue kusudi lake. Mapenzi
yake ni kwamba tuishi maisha kwa mwelekeo, maono, tukijua tunakoenda. Anatutaka
tushindane, tukiwa tumedhamiria kupokea taji – kuwa na alama, shabaha, maono ya
huko tunakoelekea.
Hata hivyo, sio tabia ya Mungu
kulazimisha maono kwa mtu yeyote. Yesu alisema, “Ombeni nanyi mtapewa.”
B.
WATU
WA MAONO WA BIBLIA
Tuchunguze
baadhi ya mifano ya ki-Biblia ya watu wa maono.
1.
Yusufu
Mwanzo
37:5-11 huelea hadithi ya maono ya Yusufu. Katika umri wa miaka kumi na saba,
alipokea maono kwa ajili ya maisha yake katika ndoto mbili Bwana alizompa.
Kwa urahisi zikisema tu kwamba atakuja
kuwa mtawala kati ya watu. Ndugu zake, baba na mama siku moja watakuja
kumsujudia na kumtumikia. Haya ni maono ya Mungu kwa Yusufu. Alipowashirikisha
maono haya, wazazi wake na ndugu zake waliyakataa.
Mwanzo 37:10 huelezea, “…Baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto
gani hii uliyoiota?” ka
tika
Mwanzo 37:8, jibu la ngudu zake Yusufu kwa maono yake kwa uwazi lilisema: “…Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto
yake, na kwa maneno yake.” Baadaye wakafanya shauri juu yake wamwue lakini
wakaishia kumwuza utumwani ili kuondokana na “ndoto” zake na maono yake.
Ni wangapi wenu mnaamini kwamba maono
yatakulete upendo wa papo hapo na heshima? Niamini, si rahisi!
Kama hadithi ya Yusufu inavyoonyesha,
maono yanaweza kukuingiza katika
matatizo makubwa sana. Hata hivyo hadithi yake ilikuwa na mwisho mwenye furaha.
Kuna kitu kinachostahili kujifunza hapa, mfano mzuri tunaohitaji kuangalia.
Maono kutoka kwa Bwana siku zote hupimwa kwa taabu na mateso.
2.
Musa
Musa,
kama Yusufu , alikuwa na maono. Kuna aya ya kufurahisha katika Matendo 7:22-25
inayoelezea yaliyotokea.
“Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri,
akawa hodari wa maneno na matendo. Umri wake ulipopata kama miaka arobaini
akaazimu moyoni kwake kwenda kuwatazama ndugu zake Waisraeli. Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipia
kisasi Yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri. Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa
mkono wake, lakini hawakufahamu.”
Mungu alimpa Musa maono, ya kuwa atakuwa
mkombozi wa watu wake. Musa alisadiki, akathubutu, akidhani, ndugu zake
wataelewa. Lakini, walielewa? Je, walielewa hata kidogo kuliko ndugu zake
Yusufu walivyoelewa? Hapana, hawakuelewa! Kweli, Maandiko yanasema, “…hawakufahamu.”
“Siku ya pili yake akawatokea walipokuwa wakishindana,
akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona
mnadhulumiana? Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema,
Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu? Je, wataka kuniua mimi
kama ulivyomwua Yule Mmisri jana?
Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya
ugeni katika nchi ya Midiani…” (Mdo 7:26-29).
Ukweli kwamba ndugu zake walishindwa
kumwelewa, haikumaanisha kuwa maono hayakutoka kwa Bwana, zaidi kuliki katika
suala la Yusufu. Maono yao yalikuwa ya
Mungu. Lakini wote wawili, ilikuwa ni lazima kupitia katika muda wa kujaribiwa.
3.
Ibrahimu
Mfano
mgumu sana wa kujaribiwa katika Agano la Kale ni ule wa maono ya Ibrahimu.
Mungu alimwambia akamtoe sadaka ya kuteketezwa mwanaye wa pekee Isaka, agizo
linaloonekana kupingana na maono ambayo Mungu alikuwa amempa.
Katika muda huo usiokuwa na matumaini, na
Isaka akiwa juu ya madhabahu, Mungu aliingilia kati na kuyafufua maono ya Ibrahimu.
Alimrudisha Isaka, na Mungu akatimiza ahadi yake kwa Ibrahimu.
4.
Paulo
Paulo alikuwa na maono. Alimwambia Mfalme
Agripa, “…Sikuyaasi yale maono ya mbinguni” (Mdo 26:19). Maono ya Paulo
alijulishwa mara tu baada ya kubadilishwa, na maisha yake mara nyingi
yalielekezwa, na maono hayo. Sisemi ‘kila mara’ kwa sababu kulikuwepo na
tofauti, na tofauti hiyo ndiyo yenye
fundisho la muhimu sana.
Sasa tunaingia katika somo la majadiliano.
Tunaelekea kufikiri kwamba watu wakuu wa Biblia kamwe hawakufanya makosa. Paulo ni mtu aliyekuwa na madhaifu na
tamaa kama tulivyo. Alikabiliwa na matatizo ambayo mimi na wewe tunakabiliana
nayo. Hakuwa mtu mwenye uwezo kupita wanadamu wengine au mtakatifu zaidi.
Alikuwa na udhaifu wa kibinadamu kama sisi sote tulivyo.
Kwa sababu ya shauku kubwa ya Paulo ya
kuona kuwa Wayahudi wanaongoka, alishindwa kudumu katika mipaka ya maono ya
Mungu kwa ajili yake. Ni kule kushindwa kwake kudumu katika mipaka ya maono ya
Mungu kwa maisha yake na huduma yake, kulikomfanya kuingia katika matatizo.
Unafikiri kuwa Paulo hakuwahi kamwe
kuingia katika matatizo? Hakika, nafikiri aliingia.
Matendo 9:15 ni tangazo la maono. Baada
ya Paulo kubadilishwa, Bwana akamwambia, “…Nenda
tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa…”
Katika Wagalatia 2:7, Paulo aliandika kuwa
alikabidhiwa injili ya wasiotahiriwa (watu wa Mataifa). Alikuwa awe mtume kwa
watu wa Mataifa na zaidi ya hayo alijua hivyo. Paulo alijua kwa ufasaha maono
ya Mungu kwa maisha yake.
Paulo aliitwa kwa ajili ya watu wa Mataifa,
lakini alikuwa ametanguliwa na shughuli nyingine. Je, ni wangapi wenu mnajua
shauku yake ilikuwa ni nini? Shauku ya Paulo ilikuwa juu ya ndugu zake
Wayahudi.
Katika Warumi 9:3-4 aliandika “Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe
niharimishwa na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi
ya mwili; ambao ni Waisraeli…”
a.
Kupokea
Katika Maono. Ni dhahiri kwamba, Paulo alikuwa
hajaridhika kabisa kuendelea na maono
aliyokuwa amepewa na Mungu kuwaleta watu wa Mataifa kwa Yesu. Kwa hivyo
tunakuta tabia ambayo tusingaliweza kuitegemea katika maisha ya mtu kama Paulo.
Paulo anasema, “Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa
rohoni” (Mdo 20:22). Hapa Paulo yupo Mileto, akiongea na Wazee wa Efeso
akiwashirikisha maneno yake ya mwisho kabla hajaondoka.
Kwa nini Paulo anakwenda Yerusalemu? Alikuwa anakwenda kwa sababu alitaka kuwaleta
Wayahudi kwa Yesu. Alitaka kuwashuhudia Wayahudi, na hivyo anasema, “Basi sasa angalieni, nashika njia kwenda
Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko;
isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na
dhiki vyaningoja” (Mdo 20:22-23).
Kwa nini Roho Mtakatifu humpa ujumbe au
humshuhudia mji kwa mji? Je, ni kwa sababu Roho Mtakatifu alitaka kumtesa kwa
vifungo na dhiki, vifungo na
minyororo? Hapana!
Roho Mtakatifu anapoanza kushuhudia kwa
namna hii katika maisha yako, ni ili kwamba uweze kufikiri tena mwelekeo wako.
Utafikiria tena utendaji wako, na
mwelekeo na kuokolewa kutokana na mateso yasiyokuwa ya lazima.
Kila mahali Paulo alikokwenda, Roho
Mtakatifu alikuwa akimshuhudia, akisema ya kuwa vifungo na dhiki vilimngoja.
Lakini Paulo hakuzuiwa na maonyo hayo. Wala hakuogopa. Alikuwa anakwenda
Yerusalemu.
Paulo alikuwa amejiweka katika njia ambayo
hakukubaliana na maono ya Mungu kwa maisha yake. “Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia
Paulo kwa uwezo wa Roho asipande kwenda Yerusalemu.” Na yeye alifahamu
nini? Paulo akaendelea kwenda
Yerusalemu!
Paulo akaendelea mpaka Kaisaria, na nabii
fulani aliyeitwa Agabo alimjia. Ni Bwana ndiye aliyemtuma Agabo kwa Paulo ili
akae kati ya Mataifa na kufanya Mapenzi ya Mungu kwa maisha yake.
Agabo atwaa mshipi wa Paulo akajifunga miguu
na mikono, akionyesha unabii wake akisema, “…Roho
Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu
mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa” (Mdo 21:11). Watu gani? Watu wa Mataifa!
Paulo alitaka kuwaleta Wayahudi kwa Yesu, lakini
maono ambayo Mungu ameanzisha kwa ajili ya maisha ya Paulo yalikuwa ni lazima
yatimilike bila kujali kama Paulo anapenda au la. Kama aliendelea kwenda
Yerusalemu, wangemfunga mikono na miguu na kumtoa kwa watu wa Mataifa.
(Kipaumbele cha kwanza cha maono na wito wake!)
b.
Uchunguzi
Wa Paulo. Paulo angeweza
kufanya uchaguzi wake. Angeweza kwenda kwa watu wa Mataifa kama mtu huru. Au,
angeweza kupuuzia maonyo ya nabii. Kama angepuuza maonyo ya ndugu waTiro na katika Kaisaria na makanisa ya watu
wote wa Mataifa, angelikwenda kwa watu wa Mataifa hali amefungwa minyororo. Je,
unajua alichagua nini?
Paulo alikwenda
Yerusalemu!
Alipokuwa akisali ndani ya hekalu akawa
katika hali ya kuzimia roho. Akamwona Yesu akimwambi, “…Hima utoke Yerusalemu upesi, kwa sabasu hawatakubali ushuhuda wako
katika habari zangu” (Mdo 22:18).
Kwa hiyo Paulo alifanya nini? Alianza
kubishana na Bwana. Alisema kufuatia hilo, “…
Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikiwafunga gerezani wale wanaokuamini
na kuwapiga katika kila sinagogi. Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa,
mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao
waliomwua.” Na Yesu alimjibu, “…Enenda
zako; kwa kuwa mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa Mataifa.”
Je, Bwana alimwambia Paulo, “Nitakutuma uende
kwa Wayahudi?” Hapana!
Je, ni kweli ulikuwa ni mpango fulani wa
Paulo wa kuwaleta Wayahudi kwa Yesu bila kujali maonyo yote, bila kujali kile
ambacho Bwana mwenyewe alimwambia Paulo?
Ungejisikia kama kupaza sauti masikioni mwa
Paulo! Watu wa Mataifa kwa Yesu, Paulo! Watu wa Mataifa kwa Yesu!”
Je, unajua ni kwa jinsi gani Paulo
alivyoondoka Yerusalemu? Kwa minyororo. Je, alitolewa kwa nani? Watu wa
Mafaifa!
Naamini Paulo angaliweza kuishi kwa uhuru
zaidi katika maisha yake kama angalidumu
katika mipaka ya maono ya Mungu, kama angalizingatia kazi yake miongoni
mwa watu wake, Wayahudi, sana na kuwa na shauku ya kuwaona wameokolewa. Naweza
kuwa nimekosea, lakini nafikiri Paulo alikosa kujua mapenzi sahihi ya Mungu
hata pamoja na kwamba Mungu alimruhusu kwenda Yerusalemu.
5.
Dumisha
Maono
Maono
ni kitu cha muhimu sana, na ni lazima kushikilia maono Mungu anayokupa.
Tunahitaji kujifunza kutokana na mifano
ya Biblia juu ya watu wa maono kama Ibrahimu, Yusufu, Musa na Paulo.
Kama mtu binafsi (au shirika au chama)
akiacha maono Mungu aliyompa, hatimaye atakwenda kukabiliana na aina ya
matatizo aliyokabiliana nayo Paulo.
Mungu anapoanzisha maono kamwe
hatabadilisha mawazo yake hata kama watu wangebadilisha mawazo yao. Bwana sio
mtu, kwamba atabadilisha mawazo yake. Wala yeye si Mwanadamu hata aweze kusema uongo.
Yeye anaposema kitu, hutegemea kifuatwe mpaka
mwisho wake! Unaweza kusema “Amina” kwa hilo?
Maono yanaweza kutimizwa, kama katika hali
ya Paulo, bila kujali kwenda nje ya maono. Uchaguzi ni kama tutafuata katika
utii na kubakia huru, au tutachukua mwelekeo mwingine wa tofauti na kuishia
katika minyororo na kifungo. Uchaguzi ni wetu. Je, utachagua matokeo ya mapenzi
yaliyoruhusiwa na Mungu? Au utachagua furaha ya mapenzi yale makamilifu?
Dumisha maono na epuka matatizo. Uwe
mkweli na mwaminifu kwa maono ya Mungu kwa maisha yako, na utakuwa na mateso
kidogo ya kuvumilia.
C.
MAONO
SAHIHI
Tunasimama
kidogo hapa kuchunguza baadhi ya mambo
muhimu kuhusu maono sahihi. Narudia tena kusisitiza kuwa maono ni muhimu sana.
Bila maono, uongozi hauwezi kutekeleza kitu chochote. Pasipo maono, watu
huangamia, watu hutangatanga, watu hukaa bila uangalifu.
1.
Maono
Huanzishwa Ki-Mungu
KWANZA,
maono sahihi ni kusudi takatifu la Mungu lililoanzishwa katika moyo wako,
katika roho yako. Yanaweza yasije katika ndoto, kama ilivyotokea kwa Yusufu.
Yanaweza yasije kama nuru inaying’ara katika barabara ya kwenda Dameski,
ikurushe kutoka juu ya punda wako, kama ilivyotokea kwa Paulo.
Yanaweza yasije kama ilivyotokea kwa Musa.
(Biblia haituelezi ni kwa jinsi gani Musa alivyotangulia kujua kwamba atakuwa
mkombozi, lakini, kwa namna fulani alifahamu!)
Maono yake yalikuja kwa upya kwa namna ya
kichaka kinachowaka moto bila kuteketea. Miaka arobaini kabla ya wakati huo
alijaribu kutekeleza maono hayo katika uwezo wake mwenyewe na alishindwa .
Yanaweza kuja kama ilivyotokea katika
maisha yangu katika maisha ya wengine wengi. Kwa miaka mingi, Mungu, kidogo
aliingiza ndani ya roho yangu maono, akinipa uthibitisho usioweza kukwepeka, na
kwamba kuna baadhi ya vitu vitakavyotekelezwa kupitia maisha yangu. Nilijua
maisha yangu ni lazima yatolewe kuwa wakfu kwa huduma fulani na huduma hizo
hazina budi kuzaliwa kutokana na maisha yangu.
Kwa namna yoyote ile maono
yatakavyokuja, ni lazima yatoke kwa Mungu.
2.
Maono
hujaribiwa
PILI,
maono hujaribiwa kwa matatizo mengi, misiba mingi. Kwa ujumla yatakuweka katika
mgongano na wengine watakaojaribu kukukatisha tamaa na kusema siyo ya Mungu.
Kila aina ya hatua itachukuliwa kunyume nawe unapoingia katika maono uliyopewa
na Mungu.
Hivyo ni sehemu ya njia ya Mungu ya kujaribu
kila maono. Neno la Bwana hujaribiwa siku zote. Hupimwa siku zote, na sehemu ya
njia ya kujaribiwa ni Bwana kuruhusu vipingamizi kuinuka kinyume nawe unapoanza
utekelezaji wa maono yake.
3.
Maono
Yana Mipaka
TATU,
tunaweza kubaki katika mipaka au kwenda
nje ya mipaka ya maono. Mungu anaweza kutupa maono, lakini baadaye tunaweza
kwenda kinyume nayo. Hii ndiyo maana halisi ya “hiari ya nia ya binadamu.”
Tunapoona mtu aliyejitoa kwa Kristo kama Paulo, akitoka nje ya mipaka ya maono
ya Mungu, sisi tuliobaki tunapaswa kuwa waangalifu. Kumpenda Bwana hakutukingi
kutokana na makosa ya juhudi zetu..
4.
Maono
Huatamiwa
NNE,
mtu anapokuwa amepokea maono kutoka kwa Bwana – na kujua hivyo – unaonekana
kuwepo kwa msukumo wa kuanza kufanya kitu, kuharakisha mambo. Sasa, mara
nyingine kunakuwepo mstari mwembamba kati ya juhudi ya Bwana na kutokuvumilia,
na naamini kuwa tunahitaji kutembea katika mstari huo kwa uangalifu.
Paulo Yongi Cho (kutoka Korea) anasema
kwamba kutolewa kwa manono ni kama inavyotokea mwungano wa mbegu ya kiume na
kike kwa yai la kuku. Baada ya hapo inamlazimu kuku kukaa juu na kuatamia mpaka
linapoanguliwa kwenye wonyesho wa uhai.
Katika hali ya mazoea, anasema Yongi Cho,
namna tunvyoatamia maono ni kwa kupitia nyakati za kufunga, maombi na
kutafakari. Tunaita katika mawazo yetu maono aliyotupa Mungu na kufikiria juu
yautimilifu na uwazi wake mpaka Mungu atakapoanza kudhihirisha undani wake.
“Nayo nchi
ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji;
Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa
maji”
(Mwa 1:2). Katika lugha ya Kiebrania, neno
hilo ‘ikatulia’ (yaani, maana ya neno rachaph ni sawa na kuku juu ya mayai
yake) moja kwa moja lina maana “iliatamia”. Mungu aliatamia juu ya uso wa maji.
Mungu alikuwa na maono kwa ajili ya dunia
yake, na yaliletwa na Roho ya Mungu kuatamia juu ya giza lililokuwa juu ya uso
wa vilindi. Kutokana na vilindi, ukatokea ulimwengu wenye kuburudisha
uliorejesha dunia ili kuwa makazi yanayofaa kwa mtu.
Je, unayo maono yaliyo wazi? Kama hauna,
hebu mngoje Bwana mpaka atakapokupatia moja. Mruhusu akushirikishe maono.
Yanakuwa mshale, mwelekeo wa kusudi la Mungu kwa maisha yako. Halafu,
yanapokuja, “atamia” juu yake, yaruhusu
yaje katika uhai kwa kuatamiwa
5.
Maono
Ni Lazima Yashirikishwe
“Bwana
akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili
aisomaye apate kuisoma kama maji” (Hab 2:2). Bwana
anasema, “Iandike njozi [maono].”
Iandike njozi.
Shirikisha wengine. Watu watataka kujua juu ya maono yako. Yanaposhirikishwa
kwa wengine, baadhi wataitwa kufanya pamoja nawe. Utaunda kikundi na kwa
kikundi, bila shaka, kazi kubwa itaweza kufanyika kuliko ambavyo ungefanya peke
yako.
Ukifanya peke yako, hutaweza kufanya kitu
cha maana katika dunia hii. Bali, mtu anayeweza kuwaandaa wengine kutekeleza
maono ya pamoja, mtu awezaye kuunda kikundi, anaweza kufanya kazi yenye maana
kwa Ufalme wa Bwana.
Biblia inasema juu ya mmoja kuwafukuza watu
elfu na wawili kuwakimbiza elfu kumi. Hiyo ni hatua kubwa! Itakuwaje kwa watatu
au wane au hamsini wote wakifanya kazi pamoja katika maono yale yale? Pengine
wangewafukuza mamilioni na kujipatia ushindi mkuu katika Jina la Bwana.
Maono yanayoweza kushirikishwa kwa uwazi ni
kitu kinachohitajika sana katika kuwahamasisha watu na fedha kwa kufanikisha
kazi ambayo Bwana anataka ifanyike.
Wakati unapoweza kushirikisha wazi wazi
lengo unalokusudia kuliendea, wengi watakuwa tayari na watataka kukusaidia mpaka utakapolifikia.
Rasilmali zitakuja.
Tatizo siyo la misaada ya kifedha, tatizo
ni viongozi ambao hawashirikishi maono na malengo.
Kutatua tatizo la misaada ya kifedha
isiyotosha, yawezekana ni moja ya matatizo marahisi ya uongozi. Kuna fedha
nyingi zaidi katika ulimwengu huu kuliko ambavyo watu wanajua ni nini cha
kufanyia. Wakati unapoanza kushirikisha maono na malengo, watu watapangana
kukusaidia kifedha na katika njia nyingine pia.
Tatizo la fedha wanalokabiliana nalo
viongozi wa kanisa na viongozi wengine wa ki-Kristo hutokea kwa sababu hawajui
wanakokwenda.
Matatizo mengi ya aina tofauti husababishwa
na ukosefu wa maono. Wakati kiongozi anapokosa maono, watu hukaa bila
uangalifu.
Kama huna maono, watu hawataki kuchanga
kwa kanisa au shirika lako. Itakupasa kushirikisha malengo na mwelekeo wako, na
mapango ulio dhahiri unapokwenda kufikia pale unapokwenda. Halafu utapata
msaada.
Nasikia malalamiko ya mara kwa mara kutoka
kwa viongozi wa Marekani ambao hawashirikishi maono. Wanasema watu wao wanatuma
fedha kwa watu na mashirika yenye huduma kwa njia ya redio na televisheni,
“kanisa la umeme” kama inavyoitwa. Unaweza kukisia ni kwa nini? Hakika unaweza.
Huduma kwa njia ya redio na televisheni
zinawashirikisha maono yao, malengo na mipango kupitia “kanisa la umeme”.
Wanayo maono, na watu hujibu.
Nawaambia viongozi wa kanisa, “Watu wa
kanisa lako wasingekuwa wanatuma fedha zao mahali pengine kama mngekuwa
mnawashirikisha maono. Wangekuwa wanawasaidia. Kama hujui unakokwenda na
wanachama wa kanisa lako hawajui unakokwenda, watakwenda kutuma fedha zao kwa
mwingine anayefahamu anakokwenda.”
Kuna kitu kimoja cha muhimu kukumbuka kama
unataka Mungu akupatie msaada kwa ajili ya huduma yako. Ukikosa kitu hiki,
unaweza ukawa unashirikisha maono yako na bado hupati msaada wa kifedha.
Ni nini hiki kitu kingine muhimu? Mungu
anatutuka tutumie fedha anazotupa kwa hekima na unyofu (uaminifu). Yeye
hataheshimu udanganyifu. Yeye hataendelea hujiahidi kwa kiongozi anayetumia kwa
upumbavu au kuishi kiutajiri kwa kutumia matoleo ya sadaka ya watu wa Mungu.
Kama wewe ni mwanamume au mwanamke wa haki,
kama utatumia fedha kwa kile ulichosema zitatumiwa kwazo, bila kuzitawanya,
Mungu atashughulika na hitaji lako la kifedha. Mungu humjali mtu ambaye ni
mwema, wa haki na uelekevu katika mwenendo wake. Yeye atamimina kwa wingi zaidi rasilmali ya
kutosha kufanya kile alichokuita kufanya. Lakini ni lazima ushirikishe maono,
na kuishi maisha yasiyo ya ubinafsi.
Tuombe
Bwana,
Yesu, fafanua kwetu leo, maono uliyo nayo kwa ajili yetu na usimruhusu hata
mmoja wetu kuondoka kutoka katika uchaguzi wa maono yako matakatifu. Tuweze
kuyakumbatia kwa furaha na mioyo yenye
utayari! Tupe neema tuyakamilishe, na tutakupa wewe shukrani katika Jina
la Yesu Kristo AMINI.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)