Alhamisi, 21 Desemba 2017

SHAHADA YA UZAMILI KATIKA HUDUMA KWA NJIA YA MTANDAO



TANGAZO
Uongozi wa   Elam Christian Harvest Seminary  kwa kushirikiana na Chuo cha GREAT COMMISSION BIBLE COLLEGE  kilichopo  MAREKANI unapenda kuwatangazia  watu wote wanaopenda kujiendeleza katika Elimu ya Mambo ya Mungu (Theology) kuwakaribisha kujiunga na masomo ya Shahada ya uzamili katika Huduma (Master of Ministry ) kwa mwaka wa masomo 2018/2019. MASOMO HAYA YANAANZA KUTOLEWA MWEZI WA KWANZA 2018
Masomo haya yanatambuliwa Kimataifa. Chuo cha Great Commission Bible College Kinatambuliwa na Bodi ya elimu ya  juu ya nchini  Marekani. Hivyo Shahada zake zinatambuliwa Kimataifa. (It is accredited Christian Institution)

Masomo  haya yanatolewa kwa njia ya Mtandao. Huna haja ya kuacha kazi zako na family yako na kwenda chuoni, masomo yetu yanakufikia kule ulipo kwa njia ya Mtandao (INTANETI) na yanafundishwa kwa lugha ya KINGEREZA
Masomo haya yametayarishwa na Waalimu mahiri katika fani ya Huduma na Theolojia, Baada ya kuhitimu mafunzo yaha mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kufanya kazi mbalimbali za kihuduma katika taasisi za kidini na jamii kwa ujumla. Mwanafunzi ataweza kushika nyazifa za uongozi katika kanisa, kufundisha Vyuo vya Biblia na Seminary za Theolojia N.k.
 MUDA WA MAFUNZO NI
Muda wa Mafunzo  ni   miaka miwili (2)  Ingawa mwanafunzi  mwenye kusoma kwa kasi anaweza kusoma kwa  muda wa chini ya miaka miwili. Mwanafunzi Atasoma Kozi moja hadi mbili kwa mwezi

SIFA ZA MWOMBAJI TUZO/AWARDS
Mwanafunzi atakayefuzu kozi zote atatunukiwa Shahada ya  UZAMILI KATIKA HUDUMA  ya  ( Master  in Ministry. M.Min) ya Chuo cha Biblia cha GREAT COMMISSION BIBLE COLLEGE   cha Marekani.

1.      Awe na  Shahada ya Theolojia au inayofanana na hiyo  awe na  angalau GPA     2.9 au Daraja  B  au
2.     Awe na Stashahada  ya juu (Advanced Diploma ) ya Theolojia  au inayofanana  na hiyo  Awe na angalau GPA ya  3.0

GHARAMA ZA MAFUNZO
       i.            Ada ya  Usajili  Tsh, 25,000/=
     ii.            Ada Ya Kila Kozi Ni Tsh,   Tsh,45,000/=
MFUMO  WA MALIPO.
Malipo yote yanafanyika kwa njia ya m-pesa kwa simu namba 0762532121

MFUMO WA UJIFUNZAJI
Mwanafunzi atatumiwa  kitabu cha kozi/Somo, mwongozo wa kozi na mtihani kwenye email yake. (barua pepe) Mwanafunzi Atasoma na kujibu mtihani, baada ya kujibu mtihani ataurudisha chuoni kwa emaili yetu ambayo ni elamexam2010@gmail.com  nasi tutaisahihisha mitihani hiyo na kurejesha majibu kwa mwanafunzi kwa njia ya email  yake.

JINSI YA KUJIUNGA
Mwombaji anapaswa kutuma  maombi kwa njia ya barua pepe kwenye emaili
Ya chuo ambayo ni elamseminary@gmail.com au  kupiga simu namba 0762532121/0765992774 kwajili ya maelekezo zaidi.
ORODHA YA MASOMO
Course Code
Course Title
Credits
EGMT 1000
Introduction to Religion
3
EGMT 1001
Attribute of God
3
EGMM 1000
Basic Christian Counseling
3
EGMM 1001
 World Mission
2
EGMM 1002
Deeper Work
3
EGMB 1001
Hebrews
2
EGMT 1003
Portrait of Jesus
3
EGMM 103
The prayer life
3
EGMB 2000
Success Through the Scriptures
3
EGMT 2000
Tenets of the Faith
2
EGMB 2000
Bible Geography
3
EGMM 2000
Understanding  your Potentials
3
EGMM 2001
Research Methods in Ministry  3
3
EGMM 2002
Biblical Hermeneutics
3
EGMT 2001
Christian Education
2
EGML 2000
Church Management and Administration
3
EGMM 2003
Thesis  
6

TOTAL Credits 50 Credits Hours
                        
LIMETOLEWA NA

Rev. Dr. Tuli.  K Brown
DEPUTY ASSOCIATE DIRECTOR GENERAL ACADEMIC AFFAIRS

Jumamosi, 20 Mei 2017

Senior Staff of Elam Christian Harvest Seminary

Elam Christian Harvest Seminary

DHANA YA UVUVIO WA BIBLIA


 MAFUNDISHO YA BIBLIA
By .Rev. Dr Erick L Mponzi

DHANA YA UVUVIO WA MAANDIKO MATAKATIFU (BIBLIA )
1. Uvuvio wa Maandiko Matakatifu.
Neno la Mungu Linanena:
Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu
walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Petro 1:21.
Kila Andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya
watu makosa yao, na kwa kuwaonya, na kuwaadhibisha katika haki. Timotheo wa
pili 3:16.

I. Maana ya Pumzi
Neno Pumzi lililotumiwa katika Timotheo wa pili 3:16 linatokana na neno la Kigriki theo Pheustos na linaonyesha ya kwamba Mungu (Theos) alipuzia (Pneo= kupuliza) Neno lake katika waandishi wa maandiko. Ni jambo la kusikitisha kujua hayo kwa maneno mawili ya Kigriki, yaliyotumiwa kwa kupumua: Peo (kupumua na  fahamu) na Psucho (kupumua polepole au bila fahamu ), Pneo linatumiwa. Pumzi,
kwa hivyo ilikuwa ni kupuzia kwa nguvu kwa fahamu na Mungu kwa mwanadamu, ambapo walipokea Neno takatifu la Mungu, kwa maneno mengine watu watakatifu wa Mungu wakiwezeshwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, na kwa utiifu wa kutosha kwa amri takatifu, kwa hivyo wakazuiliwa na kosa lolote. Kwa hali hii, maandiko yote yalitolewa na puzio

II. Aina mbalimbali za Pumzi
Sio kila anayedai kuamini katika pumzi ya Biblia, anaona upuzio jinzi tunavyoona sisi, puzio la maneno au kamili. Kwa hivyo ni muhimu kwetu kutofautisha kati ya aina mbalimbali za pumzi. Tunapotazama katika maelezo mbalimbali, itakuwa wazi ni kwanini tunaweza tu kukubali pumzi ya maneno au kamili kama “pumzi ya Kibiblia”.

1. Upuziomzi wa Asili
Haya maelezo yanakataa kwamba kuna kitu ambacho si cha kawaida, au tofauti na mengine jinsi vile Roho wa Mungu aliingia kwenye na juu ya waandishi wa maandiko. Inadai kwamba Biblia haijapuziwa kamwe kuliko vile Shakespeare, Mohamed, au Confucius.

Conn anaonyesha ya kwamba kulingana na maoni haya, ni akili ya mwanadamub kuliko Roho wa Mungu ambaye aliwazuzua waandishi wa Biblia kuandika. Hakuna kitu ambacho kingekuwa mbali na ukweli. Evans anaitikia kweli ya kwamba ikiwa hii ingekuwa tabia ya pumzi iliyo katika waandishi wa andiko, hakuna kile kinachotuhakikishia kwamba hawakuwa na uwezo wa kufanya makosa, kufundisha mambo yaleyale ya uwongo ya maisha kama vile ulivyokuwa ule mwanga wa akili yamwanadamu.
2. Upuzio usio Kamili
(1) Wazo la Upuzo wa Fikira
Hili wazo linatetea kwamba ni mawazo ya waandishi tu yalipuziwa bali si maneno. Kwa hivyo, Mungu alitoa ufunuo wake kwa dokezo lisilo pangwa sawasawa, na kuliacha kabisa kwa mwandishi kuelezea yale mawazo yaliyopulizwa. Haya yangeonyesha ya kwamba si kila neno katika Biblia lilipulizwa. Bali Neno la Mungu lenyewe linasisitiza umuhimu wa Neno moja (Mathayo 5:18). Wasimamizi wa wazo hili hawataki kufungwa na mambo ya kibiblia. Wanataka kujihifadhia wenyewe uhuru wa kutoa ufafanuzi wao wenyewe kwa maandiko. Hata
hivyo, kama si kila neno limepulizwa, tutawezaje kuamua ni maneno gani yamepulizwa na ni yapi ambayo hayajapulizwa? Ikiwa tu ni mambo ya Biblia yamepulizwa, inaweza kuwa vigumu kwetu kujua mapenzi ya Mungu.

(2) Upuzio wa Tabia na wa Kiroho
Hili jambo linaonyesha ya kwamba ni ushauri wa kiroho na kitabia katika maandikoumepulizwa.  Kwa maneno mengine, Mungu angewaachia waandishi matukio haya wenyewe, hakukuwa na hitaji la Mungu kuwapuzia. Wazo kama hilo huenda lingeacha uwezekano wa Biblia kuwa na masimulizi na makosa mengine. Kama hatuwezi kujua kikamilifu kuhusu matukio ya historia, tutakuwaje na uhakika juu ya ukweli wa kiroho? Kwa hivyo, waandishi walihitajika wapulizwe wanaponakili mambo ya historia. Pache yuko sawa anapoelezea ya kuwa shahidi ambaye haaminiwi katika njia moja hawezi kuaminiwa katika njia nyingine yoyote.

(3) Upuzio wa Kerygma
Wasomi wengi  wanashikilia wazo hili, ambalo linadhibitisha ya kwamba Biblia ina hadithi, mikasa na hadithi za kubuni. Ila wanasema ya kwamba haiwazuii kuamini katika Neno la Mungu, katika njia zao wenyewe. Kulingana na kuhitimu wazo lao hakuna mtu aliyeelimika na kuhitimu atakayekubali kwamba Biblia imepulizwa kikamilifu. Mojawapo wa wanathiolojia wenye himizo miongoni mwao akiwemo Rudolf Bultman, ambaye alihitimu kuvua Biblia miujiza yote na mambo
yasiyo ya asili. alijaribu kupunguza upuzio kwa Kerygma au mafundisho ya Biblia.Lakini haya yangemaanisha
kwamba Kuwepo kwa kwanza kwa Kristo
Kuzaliwa kwa Bikira
Uungu wa Kristo
Miujiza ya Kristo
Msamaha wa Kristo
Ufufuo wa Kristo
Kurudi kwa shangwe kwa Kristo
kama vile hukumu ya mwisho, kuwepo kwa roho wazuri na wabaya, nguvu na ubinafsi wa Roho Mtakatifu n.k. haungekuwa kweli. Ikiwa hivi ndivyo ilivyokuwa, ni kwa nini tunaamini mafundisho ya kitabu chenye maneno kuhusu miujiza, ambayo ni yenye udanganyifu mtupu.

3. Upuzio wa Kutumia Nguvu
Roho Mtakatifu, kulingana na wazo hili, alitumia waandishi wa maandiko kama mashini kuliko watu. Biblia iliamrishwa (somwa) kwa waandishi ili kwamba chochote walichoandika kilikuwa bila kosa. Hakuna nafasi iliyoachwa kwa maoni ya binafsi. Wazo kama hilo lingeonyesha ya kwamba kila kitabu katika Biblia
kimeandikwa katika mtindo mmoja, kwa sababu Mungu ndiye mwandishi wa mwisho, lakini kwamba alitoa  Neno lake kupitia kwa upuzio kwa mwanadamu wa asili, akiwakubali kuhifadhi mtindo wao wa kuandika na ubinafsi.
Tunaamini ya kwamba kila Neno katika Maandiko linatoka kwa Mungu. Lakini vilevile linaonyesha mguso wa mwandishi binadamu. Unaposoma Biblia utatambua juhudi ya kuchoma ya Paulo, utakatifu mpole wa Yohana au fikira za upole za Yakobo. Jambo ya kwamba mwandishi alizuiliwa kutokana na makosa yote  halimaanishi ya kwamba alipoteza utu wake wa mwanzoni.





4. Kamili, Ikijawa na Pumzi ya Maneno
Tunaposema kwamba tunaamini katika pumzi ya maneno (kamili) ya Biblia, tunadhibitisha ya kwamba Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa maandiko katika njia fulani, kwamba, aliwaacha na ubinafsi wao na mtindo, ili hali akiwazuia kutokana na makosa yote.
Upuzio wote unamaanisha ya kwamba upuzio ni kamili na bila chochote kuachwa!
Maandiko yanashuhudia kwa himizo hilo yanapoelezea ya kwamba “maandiko yote yanatolewa na Mungu” (Timotheo wa pili 3:16). Kila neno (lililonenwa) katika Biblia limepulizwa na Mungu. Baneroft anaelezea hivi: “ingawaje Roho Mtakatifu hakuchagua maneno kwa waandishi, ni dhahiri kwamba aliyachagua kupitia kwa
waandishi.  Mbali na jambo ya kwamba Andiko limepulizwa kikamilifu kwa maneno, hata hivyo, lina historia, na lugha ya wanadamu, hata na watenda dhambi. Katika kitabu cha Ayubu hatupati tu maneno yaliyoongelewa na Mungu, maongezi ya Ayubu  na marafiki zake, bali hata na shetani. Kwa sababu hiyo, ni maneno tu yaliyo
zungumzwa na  Mungu  yalikuwa matakatifu, bali kila neno ambalo mwandishi wa Ayubu alinakili chini ya Upuzio Mtakatifu. Kwa hivyo, kila neno lilipulizwa na Mungu. Baada ya kutambua ni nini maana ya Upuzio wa maneno, tunaweza sasa kuitikia Biblia kwa njia mpya. Kwa kila muumini aliyezaliwa mara ya pili, ni hakika. Tunaposoma ukurasa mgumu na huku kuelewa, hatutairejea kama mwanafunzi mkarimu
afanyavyo anayesema: “kuna kitu kibaya na kifungu hiki cha andiko.” Lakini badala yake tutasema: “kuna kasoro na kuelewa kwangu kwa kifungu hiki” na tutamuuliza Mungu kutusaidia katika kuelewa kwetu.

Jumapili, 12 Machi 2017

DIPLOMA YA THEOLOJIA KWA NJIA YA INTANETI



ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY
ECHASE
SEMINARI YA MAVUNO ELAM
P.O.BOX 69 MKWAJUNI   SONGWE
Tel.   0762532121. Email.  elamseminary@gmail.com

Kuwaandaa Watendakazi kwaajili ya Mavuno ya Nyakati za Mwisho.
LUKA 10:2
DIPLOMA YA BIBLIA NA THEOLOJIA KWA NJIA YA INTANETI
Uongozi wa Chuo cha Biblia cha Elam    Christian Harvest Seminary unapenda kuwa tangazia umma wote   wanaopenda kujiendeleza katika Elimu ya Mambo ya Mungu (Theolojia)  kuwa imeanzisha program ya Mafunzo ya Biblia na Theolojia kwa njia ya Mtandao (Intaneti).
Tunatoa DIPLOMA YA BIBLIA NA  THEOLOJIA kwa njia ya Mtandao
Huna haja ya kuacha kazi yako na familia yako na kwenda chuoni kwa muda mrefu, Waweza kusoma ukiwa unaendelea na kazi yako na kufikia maono yako au ngazi unayotaka.
Diploma ya Biblia na Theolojia ina jumla ya masomo/kozi arobaini na mbili (42 ) zenye jumla ya krediti tisini  (90)
Mwanafunzi aweza kusoma kuazia kozi moja hado kozi tatu kwa mwezi. Mwanafunzi atatumiwa masomo na mitihani kwenye emaili yake na baada ya kujifunza na kufanya mitihani mwanafunzi atarudisha mitihani kupitia emaili ya chuo liyoko hapo juu.
GHARAMA ZA MASOMO
Chuo chetu kinatoa mafunzo kwa gharama nafuu kabisa inayomwezesha kila mtu kumudu.  Gharama zetu hulipwa kwa kila kozi.
·        Ada ya usajiri ni Tsh. 11,000/=
·        Ada ya kozi ni  Tsh. 15,000/=
·        Mwanafunzi aweza kulipa ada ya muhula mzima au ada ya kila kozi atakayosoma kwa muda husika.





LUGHA YA MAFUNZO
Masomo yanafundishwa kwa lugha mbili  Kiswahili na Kiingereza. Mwanafunzi atachagua lugha atakayotumua katika masomo yake.

Baada ya Mwanafunzi kufuzu kozi zote 42 atatunukiwa Diploma  ya Biblia na Theolojia.
Watu wote mnakaribishwa kujiunga na chuo hiki ili muweze kuandaliwa kwaajili ya mavuno ya Kiroho.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba za simu za hapo juu au kwa barua pepe ya hapo juu.
Wako katika Mavuno


Rev. G J Kagussa
Naibu Makamu Mkurugenzi Mkuu Taaluma.
ELAM CHRISITAN HARVEST SEMINARY






ORODHA YA KOZI NGAZI YA   STASHAHADA (DIPLOMA)
Programu ya Biblia na Theologia inalenga kuwaandaa watendakazi na viongozi wa kanisa wenye kujaa  upako wa Roho mtakatifu na wenye taaluma ya kutosha katika uwanja wa theologia, huduma za kanisa na sanaa. Pia inalenga kuwapa stadi na ujuzi na kuwajengea uwezo wa kumtumikia Mungu katika wito wao kwa ufanisi mkubwa. Baada ya mafunzo haya viongozi hawa watakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utumishi wao na kuweza kumzalia Mungu matunda yanayodumu. Pia wataweza kufanya shughuli za uongozi na kutumia raslimali mbalimbali katika kuujenga ufalme wa Mungu. Pia programu hii inalenga kuwandaa wanafunzi   kitaaluma ili wawe na uwezo mpana wa kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika fani mbalimbali za elimu ya ki-Mungu.
Programu hii inajumla ya krediti 90  na  itachukua miaka  mitatu ya  ya mafunzo darasani na nje ya darasa
Baadaya kuhitimu mafunzo mwanafunzi ataweza kufanya huduma mbalimbali kutegemeana na wito  wa Mungu au huduma iliyomo ndani yake.
ORODHA YA KOZI NGAZI YA   STASHAHADA (DIPLOMA)
Mwaka Wa Kwanza
Semista ya Kwanza
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDB 100
Uchunguzi Wa Agano la Kale
3
EDB 101
Uchunguzi wa Agano Jipya
3
ED T 100
Misingi ya Imani
2
EDM 100
Sifa na ibada
1
EDT 105
Bibliolojia
2
EDB 103
Mbinu za Kujifunza Biblia
2
EDA 100
Stadi za Mawasiliano na mbinu za Usomaji
2

Semista ya Pili
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDT 200
Kuisikia sauti ya Mungu
1
EDT201
Maisha ya Kikristo
2
EDT 202
Kanuni za kufasiri Maandiko
3
EDT 203
Kanisa
2
EDM 200
Huduma ya Ukombozi na uponyaji
2
EDM 201
Mbinu  za kufanya Uinjilisti
2
EDM 202
Homiletiksi
2
EDM  203
Mazoezi ya Vitendo I
1

Mwaka Wa Pili
Semista ya tatu
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDT 300
Historia ya Kanisa
2
EDL 300
Maandalio ya Uongozi .I
2
EDM 300
Vita vya Kiroho
2
EDC 300
Mbinu za Kupanda Makanisa
3
EDT 303
Wanawake katika Huduma
2
EDT 301
Karama Za Roho Mtakatifu
2
EDB  300
Danieli na Ufunuo wa Yohana
2

Semista ya nne
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDT 400
Agano la Mungu
2
EDP400
Saikolojia ya Biblia
2
EDT 400
Mahusiano ya Kikristo
2
EDC 400
Mbinu za Mazidisho ya Kiroho
3
EDB 400
Waebrania
2
EDT 405
Theolojia I
2
EDT  406
 Maandalio ya uongozi II
2
Mwaka wa Tatu
Semista ya Tano
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDL 500
Kanuni za Uongozi wa Kiroho
2
EDM 500
Theolojia ya Utendaji
2
EDM 501
Huduma ya Masaidiano
1
EDT 500
Ndoa na Familia ya Kikristo
3
EDT 505
Utafiti wa ki-Theolojia
2
EDT 502
Theolojia II
2
EDA 500
Ujasiliamali
2
EDL 502
Mazoezi ya Vitendo II
1
Semista  ya Sita
NAMBA YA KOZI
JINA LA KOZI
KREDIDI
EDT 604
Dini zaUlimwengu
2
EDT 600
Huduma tano za Uongozi
1
EDP 600
Ushauri wa Kichungaji
3
EDT 601
Theolojia ya Kichungaji
2
EDL 600
Kuongoza kwa Kusudi
1
 EDA 600
Sayansi ya Jamii
1
EDM 600
Mbinu za Ufundishaji
2
EDT 602
Maadili ya Kichnungaji
2
EDT 606
Kupokea Upako wa Roho Mtakatifu
1