SURA
YA KWANZA
MAKUSUDI YA KUWEPO KWA KANISA DUNIANI
KANISA LINALOSHIKAMANA NA MAPIGO YA MOYO
WA MUNGU
Kanisa linaloshikamana na mapigo ya moyo
wa Mungu ni kanisa lililozaliwa moyoni mwake na linatembea na kuishi kwenye
moyo wa Mungu.
Makanisa mengi yamezaliwa kwenye mioyo
ya maaskofu, mitume, manabii, madhehebu na yanatembea ndani ya mioyo yao na sio
moyo wa Mungu.
Neno kanisa kwa lugha ya Kiyunani
linatafsiriwa kama Ecclesia maana yake waliotwa na mfalme. Ilikuwa ni desturi
kwa wayunani kwa mfalme kufanya kikao na watu wake. Na kikao hiki cha mfalme na
wale walioitwa ili wasikie toka kwa mfalme na mfalme asikie kutoka kwao.Mkutano
huu uliitwa Ecclesia.
Kwa hiyo kanisa ni kundi la watu
walioitwa na mfalme Yesu ili wasikie kutoka kwake na yeye asikie kutoka kwao.
MAMBO YA KUFAHAMU ILI UWE KANISA LINALOSHIKAMANA
NA MAPIGO YA MOYO WA MUNGU.
Ø Yesu ndio anaejenga kanisa lake.
Mathayo 16:18 “Nami nakwambia wewe ndio Petro na juu ya
mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda”
Kanisa linaloshikamana na mapigo ya moyo
wa Mungu ni kanisa linalojengwa na Yesu mweyewe.
Makanisa mengi yamejengwa na watu na
taasisi na sio Yesu aliejenga makanisa hayo, hivyo hutembea na malengo
yao na sio malengo ya Yesu kujenga kanisa lake.
Yesu hutumia watu aliowaita mwenyewe
kujenga kanisa lake, yeye hushuka na kukaa ndani ya watu hao na kuanza kujenga
kanisa lake.
1 Wakorintho 3:10-14. Kwa kadri ya neema ya Mungu niliyopewa mimi kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima
naliuweka msingi”
Ø Kanisa
ni mwili wakristo
1koritho 12: 27 “Bali ninyi
mmekuwa mwili wa kristo na viungo kila kimoja peke yake”
Kanisa kama mwili wa Kristo, unatakiwa
mwili wote uwe salama. Kama kuna kiungo kimoja kina shida mwili wote hauwezi
kuwa salama. Hivyo kila kiungo kina umuhimu wake kuwa salama kwa afya ya mwili
wote. Mfano mfumo wa damu, uti wa mgongo, ubongo, mfumo wa upumuaji, tumbo la
usagaji wa chakula. Kimoja kati ya hivyo kikisumbua mwili wote husumbua maana
Mungu aliweka vyote kwa makusudi.
Mungu ameliweka kanisa kwa makusudi
yake. Makusudi ya kanisa ndio yanayolifanya kanisa liwepo na liwe na afya na
kukua, na kama makusudi hayo yakafanywa yote
na Moja likapungua basi afya ya kanisa itateteleka.
Ø Kutambua kuhusu AMRI KUU na AGIZO KUU. Katika agano
jipya.
Ndani ya amri kuu tunapata makusudi mawili
ya kanisa kuwepo duniani na ndani ya agizo kuu tunapata mambo au makusudi
matatu ya kanisa kuwepo.
Mathayo
22:36-40 “Mwalimu, katika torati ni amri
ipi iliyo kuu”? Akamwambi “mpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako
wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote. Hii ndio amri iliyo kuu tena ni
ya kwanza nayapili yafanana nayo
ni hii mpende jirani yako kama nafsi yako katika amri hizi hutegemea torati
yote na manabii”
Biblia
yote imefupishwa katika kifungu hiki cha maandiko, hivyo ni lazima kanisa
litembee katika kifungu hiki. Likifanya hivyo litakuwa limetembea sawasawa na
Biblia.
Ø
Katika
amri kuu tunapata makusudi makuu mawili ya kanisa kuwepo ambayo ni:-
i.
Kuabudu. Kuabudu ni
kuonesha upendo kwa Mungu, lengo la kwanza la kanisa ni kupeleka sifa kwa
Mungu. Na huku ndio kumpenda Mungu kwa moyo wote (Mathayo 22:27)
ii.
Huduma Matyho 22 :29 “Mpende jirani yako kama nafsi yako”
Waefeso 4 :12, “Kwa kusudi la kuwakamilisha
watakatifu hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa kristo ujengwe”
Kusudi la kanisa tunalolipata katika
amri kuu ni kuwakamilisha watakatifu ili wafanye huduma, Mtakatifu bila kujua
vipawa vyake na huduma yake ndani ya kanisa na jamii anakuwa hajakamilika.
Hayo ndio makusudi mawili ya kanisa
tunayoyapata katika amri kuu.
Ø
Makusudi matatu
tunayoyapata katika agizo kuu ni
Mathayo 28:19-20.
“Basi
enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa
wanafunzi, mkiwabatiza kwa jia la baba na Mwana na Roho Mtakatifu na
kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Tazama mimi nipo pamoja nayi
hata ukamilifu wa dahari”.
Katika agizo kuu pia tunapata makusudi
matatu ya kanisa ambayo ni :-
Uinjilisti, ushirika na uanafunzi.
Ø Hivyo
makusudi matano ya kanisa linalogusa
moyo wa Mungu ni
i.
Kuabudu
ii.
Huduma
iii.
Uinjilisti
iv.
Ushirika
v.
Uanafunzi
Yohana 17:4-15 “Mimi nimekutukuza
duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
Ø Kusudi la kwanza
kuabudu.( 17:4)
Ø Kusudi la pili
Uinjilisti (17:6)
Ø Kusudi la tatuUinjilisti
(17:8)
Ø Kusudi lanneUshirika
(17:12)
Ø Kusudi la tano Huduma
(17:13-15)
Matendo ya mitume 2:41-47.
Hapa napo tunaona kanisa la kwanza
likitembea nahayo makusudi matano ya kanisa kuwepo duniani. Waefeso 4:11-16
KUKUA KWA KANISA
Katika kipengere hiki tutaangalia kwa
upana kuhusiana na mambo matatu yaliyopo ndani ya agizo kuu ambayo ni
uinjilisti, uanafunzi na ushirika.
Mathayo 28:19-20
“Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa
wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu na
kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Tazama mimi nipo pamoja nanyi siku
zote hata ukamilifu wa dahari”.
Mwanafunzi ni mtu anaeingia darasan ili
ajifunze siku kwa siku na hatua kwa hatua.
Kwa hiyo kanisa ni kundi la wanafunzi wa Yesu wanaojifunza kuyashika na
kuyatii mambo yote aliyoyaagiza Yesu hatua kwa hatua na siku kwa siku.
Kwa maneno mengine tunaweza kueleza
kwamba kanisa ni shule ya kiungu.
Kuna mambo mengi yanayofanya shule kuwa
na ubora. Baadhi ya mambo hayo ni
Uwepo wa walimu bora, ubora wa elimu,
matunda ya elimu inayotolewa na wingi wa wanafunzi.
Hivyo kanisa lenye ubora pia ni kanisa lenye
wanafunzi wengi wa Yesu Kristo wakiwa mahali pamoja kujifunza na kutii mambo
yote aliyowaamuru Yesu. Hivyo kanisa lenye idadi kubwa ya wanafunzi ni mpango
wa Mungu. Ni mojawapo ya ufanisi wa shule ya Yesu. Hivyo ni mapenzi ya Mungu
tuwe wengi kanisani.
Kanisa lenye watu wengi maana yake ni
watu wengi wamesamehewa dhambi, watu wengi wanakwenda mbinguni, Unjilisti
mwingi umefanyika, sifa nyingi zina mwendea Mungu.
Mifano ya mikusanyiko ya kanisa la
mahali pamoja katika Biblia.
i.
Kanisa la
jangwani.
Matendo ya Mitume 7:38 “Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa
jangwani pamoja na Yule malaika aliyesema nae katika mlima Sinai, tena pamoja
na baba zetu, ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi”
Wana wa Israeli ndio waliokuwa kanisa la
jangwani, pamoja na mchungaji wao Musa
Ø
Je Kanisa la
jangwani lilikuwa na watu wangapi ?
Kutoka 12:37 “Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramasesi mpaka Sukothi wapata hesabu
yao kama watu mia sita elfu watu waume waliokwenda kwa miguu bila kuwahesabu
watoto
ii.
Kanisa wakati wa
Yesu:-
1Petro
2:21 “Kwa sababu ndio mlioitiwa kwa maana
Kristo nae aliteswa kwaajili yenu akawaachia kielelezo mfuate nyayo zake”
Hivyo Yesu ndio kielelezo chetu ambaye tunatakiwa kumfuata
vile alivyofanya.
Luka 12:1 “Wakati
huo makutano walipokutanika elfuelfu hata wakakanyagana alianza kuwaambia
wanafunzi wake kwamba jilindeni na chachu ya mafalisayo ambayo ni unafiki”
Kwenye huduma ya
Yesu walikusanyika maelfu ya watu na sio mamia ya watu.
Mathayo
14:21 “Nao waliokula walikuwa wanaue
wapata elfu tano bila wanawake na watoto”
iii.
Kanisa wakati wa
mitume
Marko 3:13-19 Yesu aliwatuma wanafunzi
12
Luka
10:1 Baada ya huduma kuongezeka
akawatuma wengine sabini.
Matendo ya mitume 2:41 “ Nao waliolipokea lile neno lake wakabatizwa
na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu”
Matendo ya mitume 4:4 “lakini wengi
katika hao waliolisikia lile Neno waliamini na hesabu yao watu wanaume ikawa
kama elfu tano”
Matendo ya mitume16:3 “Makanisa yakatiwa
nguvu katika ile imani hesabu yao ikaongezeka kila siku.
Kumbe kanisa lenye idadi kubwa ya wanafunzi ni
moja ya sifa ya kanisa linaloshikamana na mapigo ya moyo wa Mungu.
SURA
YA TATU
NAMNA
YA KUJENGA KANISALINALOSHIKAMANA NA MAPIGO YA MOYO WA MUNGU
A. NIA YA KRISTO
Kuna mambo mengi yanayoweza
kukuwezesha kujenga kanisa linaloshikamana na mapigo ya moyo wa Mungu. Baadhi
ya mambo hayo ni:-
1. kubadili nia
yako na mtazamo wako
Mtazamo ni mawazo yako binafsi kuelekea jambo fulani ,mtazamo ni jinsi unavyoyaangalia
mambo au jinsi unavyoyachukulia mambo, unavyoyatafsiri mambo na kuyapa majina
husika. Mtazamo ni hukumu yako binafsi kuelekea jambo fulani, mtazamo wako juu
ya jambo fulani waweza kukujenga au kubomoa, ukibomoka au kuharibiwa kwa jinsi
hii utakuwa haukubomolewa na shetani
bali mtazamo wako umekubomoa.
Kwahiyo ili kujenga kanisa linalompendeza
Mungu lazima ubadili nia na mtazamo wako kuhusu kanisa na kuyakataa mapokeo
yote uliyoyapokea na yakaweka mizizi ndani ya ufahamu wako lakini sio ya ki-Biblia.
Wafilipi 2:5 “Iweni na nia hiyohiyo ndani yenu,ambayo ilikuwemo ndani ya Kristo Yesu”
Unatakiwa
kuwa na nia iliyokuwa ndani ya kristo. Achana na nia za wanadamu
Wakoritho2:16 “ni nani aliyefahamu nia ya Bwana amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya
Kristo”
Ili uwe kanisa linalompendeza Mungu lazim ujue
nia na mtazamo wa kristo na vikae ndani yako daima.
Ø
NIA YA KRISTO NI
IPI ?
Neno nia limetafsiriwa kama idara ya fikra
au mawazo ndani ya mwanadamu. hivyo kubadili nia ni kubadili namna ya
kufikiri,lazima tuwe na nia ya kristo ambayo ni
i.
Nia
ya kristo ni kuwa hapendi mtu yoyote apotee bali wote waifikie toba
1Petro3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kama wengine wanavyokudhania kukawia
bali huvumilia kwenu, maana hapend mtu yeyote apotee bali wote wafikilie toba”
Watu wote kwenye mtaa, kijijini
kwako,ofisini, shuleni,kazini, ukoo wako hataki hata mmoja apotee.
ii.
Ni nia na
mtazamo wa kristo kuwataka watu wote waokolewe 1Timotheo 2:3-4 “hili nalo ni zuri lakubarika mbele za Mungu
mwokozi wetu ambaye hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyokweli”
Vaa nia
na mtazamo huu kwamba Mungu anataka kila unayemwona lazima aokolewe ndio yawe
maombi yako na juhudi yako.
iii.
Nia na mtazamo wa Yesu anawaagiza watu wote wa kila
mahali watubu Matendo ya mitume 17:30 “basi
zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni bali sasa anawaagiza watu
wote wa kila mahali watubu”
Maombi yako watu
wote wa mji wako wanaokuzunguka waamuru wapate kutubu.
iv.
Ni
nia na mtazamo wa Mungu kwamba neema yake ya wokovu imefunuliwa kwa wanadamu
wote.
Tito
2:11 “maana neema ya mungu iwaokowayo
wanadamu wote imefunuliwa”
Haijalishi
watu wako vibaya kiasi gani wewe fahamu tu neema ya Mungu imefunuliwa kwa wote.
v.
Nia
na mtazamo wa Mungu ni kwamba jehanamu ya moto haikuandaliwa kwaajili ya watu,
ameandaliwa shetani na malaika zake.
Mathayo25:41 “kisha atawaambia wale
walioko mkono wa kushoto,ondokeni kwangu mliolaaniwa mwende katika moto wa
milele uliowekwa tayari kwaajili ya ibilisi na malaika zake”
vi.
Nia
na mtazamo wa kristo ni kwamba katika kristo wote watahuishwa.
Wakorintho 15:22 “kwakuwa kama katika Adamu wote wanakufa kadharika katika kristo wote
watahuishwa”
vii.
Ni nia ya Kristo kwamba mkutano mkubwa sana
usioweza kuhesabika ,watu wa kila taifa
na kabila,jamaa na lugha wasimame mbele ya kiti cha enzi na mbele ya
mwanakondoo wamevikwa mavazi meupe na matawi
ya mitende mikononi mwao. (Ufunuo wa Yohana7:9)
B. KUWA NA AFYA YA KUZAA.
Baada ya kuangalia nia ya Kristo ni ipi na mtazamo wake, umebadilika kinachotakiwa
ni kuwa na afya ili uweze kuzaa watoto wenye afya. Fahamu kwamba Mzazi
mwenye afya bora huzaa mtoto mwenye afya nzuri, na kama afya ya mzazi ni mbaya
wazazi hushauliwa kushughulikia afya zao kabla ya kuzaa.
Hivyo ni muhimu kuwa na kanisa lenye
afya ambalo litazaa wanafunzi wenye afya.
Biblia inazungumzia sana habari za
ujenzi wa kanisa ukifananishwa na ujenzi wa nyumba1Timotheo 3:15
Kila ujenzi unagharama zake, Luka14:28-30 “Maana ninani katika ninyi kama akitaka
kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kumalizia,
asije akashindwa kuumalizia baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza
kumdhihaki wakisema mtu huyu alianza kujenga akawa hana nguvu za kumalizia.”
Tangu
unapoanza kujenga ni lazima ujue ukubwa wa nyumba unayotaka kujenga ili uweke
msingi na nguzo zinazofanana na ukubwa wa jengo.
Katika kanisa msingi wake ninini?
Mathayo 7:14 “msingi wa mwamba na
mchanga
Ø
Asikiae
Neno na kutenda ni mwamba
Ø
Asikiae
Neno bila kutenda ni mchanga.
Neno
la Mungu ni mwamba wa kanisa, ni lazima kanisa lijengwe katika msingi wa Neno.
Mathayo 16:18 “Nami
nakuambia kwamba wewe ndio Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu
wala milango ya kuzimu haitalishinda”
1Wakorintho 3:11-13“Maana hakuna mtu awezae kuweka msingi mwingine isipokuwa
uliowekwa yaani Krsto Yesu”
Maana ya pili ya msingi wa Kanisa ni
wale washirika unaoanza kanisa pamoja nao.
Ø
Usimchukue
kiongozi wa kanisa lingine na kumfanya kuwa kiongozi katika kanisa lako,
haijalishi ni mzuri kiasi gani, baadae atakusumbua tu.
Ø
Anza
kanisa na watu wasio na msingi wowote, yaani wametoka dhambini.
Ø
Ukimchukua
kiongozi wa kanisa lingine na kumfanya kuwa kiongozi katika kanisa lako bila
kumfundisha, ujue unajenga kwenye msingi wa mtu mwingine.
Warumi 15:20 “kadharika nikijitahidi kuhubiri Injili nisihubiri hapoambapo jina la
kristo limekwisha tajwa, nisije ikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine”
Ø Ni salama kuanza
na wanafunzi wako mwenyewe usichukue watu kutoka katika kanisa lingine na
kuanza nao.
Ø Ikitokea mtu
ametoka katika kanisa lingine lazima awe tayari kufundishwa upya.
Baadhi ya Wanafunzi wa Yesu walikuwa ni
wanafunzi wa Yohana Mbatizaji, walipoingia kwenye huduma ya Yesu walifundishwa
kwa upya kwa miaka mitatu na nusu.
Yohana 1: 35 Wanafunzi wawili wa Yohana
wakamfuata Yesu, kwa hiyo msingi wa kanisa ni kuanza na NENO na WANAFUNZI WAKO.
Katika ujenzi baada ya kuimarisha msingi
kutatakiwa kuimarisha nguzo.
Katika KANISA NGUZO NININI ?
Mithali 9:1 “Hekima ameijenga nyumba yake, amezichonga nguzo zake saba”
Hekima ni Yesu 1Wakorintho 1:24 “nguvu
ya Mungu na Hekima ya Mungu”
Nyumba
ni kanisa nguzo ni viongozi
Wagalatia 3:9 “ Tena walipokwisha kuijua
neema niliyopewa , Yakobo kefa na Petro wenye sifa ya kuwa ni nguzo walinipa
mimi na Balnaba mkono wa kuume wa shirika ili sisi twende kwa mataifa na wao
waende kwa watu wa tohara”
Yesu alianza na viongozi 12 Marko 3:13-19
Huduma ilipoongozeka akaweka wengine 70 Luka 10:1
Mpaka
Yesu anaondoka duniani aliacha watendakazi
500.
1Wakritho15:16
Baadae aliwatokea ndugu zaidi ya 500
Matendo
1:15 Watu120 ndio walisubiri Ujazo wa Roho Mtakatifu.
Nguzo ndio husababisha afya ya kanisa na
husababisha kuzaa watoto wenye afya kizazi hadi kizazi.
Baada ya kuweka msingi, nguzo na hekima kinachofuata
ni kuambatana au ushirika kati ya hekima, nguzo na mawe.
Ushirika tunapata katika agizo kuu kwa
namna ya kuambatana Waefeso 4:1-6
Kuambatana maana yake ni shikana,
gandamana, ng’ang’aniana bila kuachana.
Kuambatana ni kutoka kwenye hali ya kuwa
vitu viwili, vitatu, vine na kuwa kitu kimoja.
Ø
Mwanzo
2:24 “Ataambatana na mkewe”
Ø Mwanzo 34:3 “ Moyo wake ukaambataa na Dina”
Ø Ruth 1:14 Akaambatana nae”
Ø 1Samweli 18:1 “Roho ya Yonathani ikaambatana na roho ya Daudi”
Ø 2Samweli 20:2 “Mkono wake ukaambatana “
Ø Mathayo 19:5 na
Waefeso 5:13 “ kuambatana mke na mme”
C.
SILAHA KUBWA
ANAYOTUMIA SHETANI KUONDOA AFYA YA KANISA
i.
Kuondoa
roho ya ushirika, umoja na kuambatana.
ii.
Kushambulia
kutoka ndani ili wale wa ndani wafungue mlango wa nje waingie.
iii.
Shetani
anayetoka nje hana nguvu ikiwa hatapewa ruhusa ya kuingia Yohana 14:30 “Yuaja mkuu wa ulimweng lakini hana kitu
kwangu”
Kama umekaa
vizuri na Bwana shetani kutoka nje hawezi kukushambulia na kukushinda. Yesu alishambuliwa
kwa kupitia mwanafunzi wake Yuda Iskariote Luka 22:3, Mathayo 10:36
D. NAMNA YA KUONDOA VITA YA NDANI.
Kuna mbinu
mbalimbali ambazo zaweza kutumika katika kuimaliza vita ya ndani, baadhi ya
mbinu hizo ni:-
i.
Kumwondoa
wakala wa vita aliyendani.
Mithali 22:10 “ Mtupe nje mwenye dharau na fitina itakoma”
Tito 3:10 “ Mtu mzushi umkatae”
Asiyeambatana na
kiongozi ni adui wa kiongozi. Hakuna kuwa katikati Mathayo 12:30 “ Asiye
pamoja nami yu Kinyume changu”
Washirika
wanapoambatana na mchungaji upendo unajaa kanisani na Yesu anatukuzwa sana.
Yohana 13:35 “Pendaneni ninyi kwa ninyi”
Kwa kawaida
kondoo hunywa maji yaliyotulia na sio
yenye mawimbimawimbi Zaburi 23:2
Uinjilisti huwa
na mafanikio kama wanafunzi watambatana na kiongozi mkuu.
Ø Mathayo 15:30 “wakamwendea makutano mengi wakamletea viwete, vipofu,mabubu, vilema na wengine wengi wakawaweka miguuni
pake akawaponya hata ule mkutano wakastaajabu walipowaona mabubu wanasema,
vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, vipofu wanaona wakamtukuza Mungu wa
Israeli”
Ø Marko 2:4 “ na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu
ya makutano walitoboa dari pale alipokuwapo”
Ø Luka 22:28-29 “Walidumu pamoja nami hata wakati
wa majaribu”
E. HATUA
SABA ZA MTU ALIYEACHA KUAMBATANA AU KUELEKEA UASI.
Kuna dalili
nyingi ambazo huonesha kwamba mtu huyu anaelekea kuasi au tayari kaasi. Unaweza
kumtambua mtu anaeelekea kuasi kwa kuchunguza
mambo yafuatayo:-
1.
ROHO YA KUJIPANGIA AU KUTENDA KAMA APENDAVYO,
Anatii yale anayoyaona yeye kuwa ni ya
muhimu
2Samweli 3:20-21 “Daudi alimsamehe
Abneri lakini Yoabu akamfuata na kumuua njiani”
2 Samweli 3:26-27
Huwa hawaondoki ila wanajipangia
wenyewe.
2.
KUJIKWAA NA KUKWAZIKA.
Mathayo 24:10 “ ndipo wengi watakapo jikwaa na watasalitiana na kuchukiana”
Anakuwa mtu wa kukwazika mara kwa mara, hata mambo ambayo zamani yalikuwa hayamkwazi sasa yanaanza kumkwaza.
Luka 17:1 “Jifunze kusamehe maana makwazo hayana budi kuja”
Kujikwaa na kukwazika
hufungua mlango wa chuki, watu wenye majeraha ni rahisi kuwa waasi”
Mfano ABSALOMU
i.
Alikuwa
na mejeraha yasiyopona juu ya dada yake Tamari kubwaka na kaka yake Amnoni
2Samweli 13:1 -22
ii.
Baba
yake(Daudi) hakuchukua hatua yoyote 2Samweli 13:21 aliishia kukasirika bila ya kuchukua hatua
yoyote sawaswa na Mambo ya Walawi 20:17. Adhabu yake:-
3.
KUTOJIHUSISHA
NA LOLOTE.
Anaacha kuja kwenye maombi na kazi za
kanisa. (Yeremia 48:10)
Hahusiki kufanya lolote, anabaki kukosoa
tu wanayofanya wengine.
4.
KUKOSOA.
Anaacha
kujihusisha badala yake anaanza kuona makosa na kuyakuza.
Anaaza kuona
makosa kweye Neno linavyohubiriwa.
Ataona makosa
kwenye utaratibu wa ibada, jinsi jengo lilivyo na utaratibu wa ibada.
Miriamu alianza
kumkosoa Musa Hesabu 12:1 “kisha Miriamu
na Haruni wakamnenea Musa”
Absalomu alianza
kuyaona makosa ya uongozi wa Daudi (2Samweli 15:3)
5.
HATUA YA KISIASA
Kuwahusisha
wengine kwenye mambo yako na malalmiko yako.
(2 Samweli 15:3) “Mchungaji
wetu mzuri lakini hashauriki hebu tumuombee “
Watu wasioambatana na kiongozi hupenda kushirikisha
wengine mapungufu ya kiongozi wao.
Maswali yao ;
Ø Umeonaje ibada
ya leo ?
Ø Unajua
haijachangamka sana eti !
Ø Wengi wanahama
hivi ni kwanini ?
Ø Mchungaji
anaendeleaje ? anajibu yupo tu .
Ø Kanisa
linaendeleaje ? anajibu lipo tu.
Ukichelewa
kumwondoa Absalomu utasikia anakwenda Hebroni kuondoa nadhiri (2 Samweli
15:7-10)
Mshauri mkuu nae
wa Daudi akajiunga na Absalomu (2 Samweli 15:12)
Ahithoferi
mshauri wa Daudi akawa mshauri wa Absalomu (2Samweli 16:23)
6.
KUDANGANYIKA
Yohana 8:44 “Shetani
ni baba wa uongo”
Unaweza kuwa na
watu wengi wa kukutia moyo, maarifa au ujuzi na uwezo wa hayo ndio yanayoweza kukudanganya
na ukawa mwasi.
Yohana 14:12 “ Utafanya kazi kubwa kuliko hizi”
Ni kweli Mungu anaweza
kukutumia sana lakin usidanganyike.
Yohana 13:16 “ Amini amini nawambia ninyi mtumwa si mkubwa
kuliko bwana wake wala mtumwa si mkubwa
kuliko aliyempeleka”
Usimdharau
mwalimu wako hata siku moja kwa kudanganywa na mafanikio fulani fulani
uliyoyafikia.
Shetani
alijidanganya alisahau uzuri aliokuwa nao kuwa ulitoka kwa Bwana Ezekieli 28:12-17
Kujidangaya
zaidi ni pale ambapo muasi anaona kuwa
anaweza kummaliza baba yake wa kiroh kwa maneno ya dini au uvumi wa uongo.
Uvumi wa uongo ni hatari sana.
Mithali 30 :7 “ mwana amdharauye baba au mamaye kunguru ataling’oa jicho lake”
7.
UASI WA WAZIWAZI.
Ni hatua ambapo wale waliodanganywa wanaanza
kupambana moja kwa moja na mamlaka.
Ufunuo wa Yohana 12:4 “ na mkia
wake wakokota theruthi ya nyota za
Mbinguni”
Ufunuo wa Yohana
1: 20 “ zile nyota ni malaika saba”
i.
Shetani
aliasi waziwazi kinyume cha Mungu (Ufunuo 7:12)
ii.
Absalomu
akapambana na baba yake
2Samweli 16:11 “Angalieni huyu mwanangu aliyetoka katika
viuno vyangu anatafuta uhai wangu”
iii.
Absalomu akachukua nafasi ya baba yake mpaka
kitandani (2 Samweli 16: 22)
iv.
Yuda kumsaliti Yesu(Mathayo
26:47-48)
v.
Kora,Dathani na
Abiramu na viongozi wengine 250 waliasi waziwazi kinyume cha Musa. (Hesabu 16:)
F.
HUKUMU YA UASI
Mwisho wa waasi
huwa ni mmoja na wa aina moja.
1 Samweli 15:11, “Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, kuasi ni kama ukafiri na
vinyago. Kwa kuwa umelikataa Neno la
Bwana yeye nae amekukataa usiwe mfalme”
Kama kuasi ni
sawa na dhambi ya uchawi Maandiko yanaagiza kwamba usimwache mchawi kuishi.
Mungu haungi mkono uasi wa aina yoyote ile
2 Samweli 15:11
“ na watu walioalikwa wakafika Yerusaleu
pamoja na Absalomu wakaenda katika ujinga wao wasijue lolote”
Ø Shetani Ufuo
12:9 “akatupwa hata nchi”
Ø Absalomu 2 Samweli 18:15 “ wakamwangukia
wakampiga Absalomu na kuuawa”
Ø Ahithoferi 2
Sawemli 17:12 “Alijiua”
Ø Adonia 1 Wafalme
2:25 “ akampiga hata kufa”
NAMNA YA KULETA
ROHO YA KUAMBATANA.
Kuna mbinu
mbalimbali ambazo zaweza kutumika katika kuleta roho ya kuambatana kati ya
kiongozi na washirika, baadhi ya mbinu hizo ni :-
i.
Endelea kuondoa
watu wasio ambatana na kiongozi haraka.
1koritho 5:6 “Chachu kidogo huchachua donge zima”
kama mtu
anaonyesha dalili ya kuondoka na aondoke haraka akibaki anaweza
kupandikiza roho
ya chuki kwa watu wengine.
Yohana 13:27 “Na baada ya hilo tonge shetani akamwingia,
Basi Yesu akamwambia uyatendayo uyatende upesi”
ii.
Tengeneza moto
ili kupima mioyo
Matendo 28:3 “Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni na kuuweka motoni nyoka
akatoka kwaajili ya ule moto akasongasonga mkononi”
Paulo aligundua alipoweka motoni kuwa
moja ya iliyoonekana kama kuni ilikuwa ni nyoka.
Ø Tengeneza wakati
mgumu ili ujue moyo wa mtu
Ø Usiwe na haraka
ya kuwapandisha vyeo, Mtu akiasi kwa sababu hana cheo maana yake angeasi pia
baada ya kupata cheo.
Ø Jaribu kutoa
uhamisho wa idara ili kupima mioyo.
Ø Fanya kazi na watu
wenye nia ya kazi pekee.
Ø Tengeneza
mazingira ya watu kuondoka kama wanapenda kuondoka
Ø Fundisha kwa
nguvu sana kuhusu kuambatana.
2Kor 8:12 “ Maana kama nia ipo hukubaliwa kwa kadri ya
alivyonavyo mtu si kwa kadri ya asivyokuwa navyo mtu”
G. UKWELI KUHUSU KUAMBATANA
Unapotaka
kuambatana na kiongozi wako ni lazima umwamini kwamba Mungu amemchagua na
uamini anavyosema siyo watu wanavyosema.
a.
Yesu
nae alilaumiwa
Luka 23:22 “ wakaanza kumshitaki wakisema tumemuona
huyu akipotosha taifa letu na kuwazuia watu wasimpe kaisari kodi, akisema yeye
mwenyewe ni Kristo mfalme”
Yesu mwenyewe
alilaumiwa kuwa,
Ø Anapotosha watu
Ø
Anawaambia
wasilipe kodi
Ø
Anadai
ni mfalme
Ø Anatoa pepo kupitia
nguvu za shetani (luka 11:15)
b.
Paulo
alilaumiwa,
Matendo 24:5-6 “kwa maana tumemuona mtu huyu mkorofi,
mwanzilishi wa fitina katika wayahudi wote duniani”
Mathayo 12:30 “ asiye pamoja nami yu kinyume change”
H. KANUNI ZA KUAMBATANA
1.
kuambatana
kwetu lazima kuwe ni kuambatana na mamlaka iliyo kuu
1wakoritho 11:1 “mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo”
Kama unatafuta
wa kuambatana naye ambatana na kiongozi mkuu daima
Warumi 13:1“ kila mtu na aitii mamlaka iliyokuu, kwa
maana hakuna mamlika isiyotoka kwa mungu”
2.
Anayeambatana
hawezi kuficha taarifa
Utamtambua mtu
kuwa ameambatana na wewe kama atakuambia taarifa za watu waharibifu.
1Wakoritho 5:1 “ nimearifiwa habari zenu kwamba iko fitina
kwenu”
Paulo alialifiwa
kwamba kuna uzinzi kanisani.
1Wakoritho 1:11” nimearifiwa habari zenu kwamba iko fitina kwenu”
Esta 2:21-22 Modekai
alipata taarifa kuwa kuna mauti naye akapata taarifa”
Matendo23:12-17” Paulo alipewa taarifa na mjomba wake
kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamue Paulo.
3.
Kuambatana kuwe
kimaandiko na sio kihisia
Ø
mtu
akihubiri vizuri ndio uambatane nae
Ø
Akiponya
wagonjwa ndio uambatane nae
Ø
Unaambatana
na mtu ambaye Biblia inamtaja kwamba uambatane nae sio hisia au mkumbo mkumbo.
Ø
Yonathani
hakuambatana na Sauli ingawa alikuwa
baba yake mzazi. Aliambatana na daudi
maana alijuwa kuwa huyo ndiye aliyepakwa mafuta kuwa mfalme. (1Sam 20:13)
4.
Kuambatana kuna gharama.
Ø
Luka
14:26, 1Samweli 20:32-33 (Yonathani).
Ø
Waebrania
11:24:26 Musa alikataa kuitwa mwana wa binti Farao.
I.
MAMBO YANAYOTOKA
KATIKA KINYWA CHA MTU ASIYEAMBATANA NA MCHUNGAJI.
1.
Si
ni kwa unyenyekevu tu lakini wengine tunaweza kabisa kuwa wachungaji.
2. Anakuja mgeni
anamtafuta mchungaji anauliza unashida gani ? Mgeni anajibu “nataka kumweleza mchungaji tu” ndio
maana hamponi.
3.
Mngejua
niliyoonyeshwa msingeendelea na maombi.
4.
Mimi
huko siji na hakuna la kunifanya. Hesabu 16:12
5.
Unaonaje
jambo hili hivi ni Biblia ?
6.
Akiwa
hayupo tunakuwa huru sana.
7.
Yeye sio Mungu naye ni mtu tu.
8.
Watu
wanamwogopa mimi simwogopi.
9.
Anasifia
kanisa jingine.
J.
TABIA ZA MSHIRIKA MWENYE KUAMBATANA NA
KIONGOZI WAKE
i.
Mtaje mchungaji wako mara nyingi
kwenye mambo mazuri.
Kila unapofundisha,
kuhubiri au unaposhauri na mifano ya miujiza ulioona Bwana Yesu anamtumia.
ii.
Mnukuu kiongozi wako mara nyingi
unapokuwa unaongelea mambo ya Mungu. Kanuni ni kwamba kadri unavyomwinua
kiongozi wako ndivyo na wewe unainuliwa.
Yohana
12:32 “nitakapoinuliwa juu nitawavuta
wote waje kwangu”
Ø Usimnukuu
kwa mambo mabaya bali mnukuu kwa mambo unayoyapenda na kuyatamani. “ kila
ufanyacho fanya kwa niaba ya kiongozi”
Ø Ukitembelea,
tembelea kwa niaba, sema mchungaji amenituma na anakupenda ameshindwa kuja anadharura.
Ø Huduma
au kanisa linatakiwa kuwa na kichwa kimoja tu ambacho ni Yesu na mwakilishi
wake ni mchungaji, hivyo usipoenda kwenye huduma kwa niaba ya mchungaji
unatengeneza vichwa kwenye huduma, na kila chenye vichwa viwili ni JITU na sio mwili wa kristo tena.
iii.
Mpende mchungaji wako na msifie mara zote.
Ø Siri
kubwa ya kupata upako ni kuwapenda na kuwaongelea vyema wenye upako.
Ø Kama
unawapenda sana viongozi wengine na huduma zingine na humpendi na kumsifia wa
kwako, fahamu kuwa hauko mahali sahihi.
iv.
Mkaribishe mchungaji wako kwa
namna ya (kumsifia) kuvutia. Vipongeze na kuvisifia vitu alivyokufundisha na
vikakugusa .
Ø Anaporudi
toka safari tangaza kwa furaha na kwa
mvuto mkubwa.
Ø “Nifuraha yetu kubwa kumwona baba yetu”
v.
Usiwe kituo cha kupoke malalamiko
na manung’uniko.
Ø Wafanye
watu wafahamu ikiwa wanataka kusengenya au kumsema mchungaji basi sio kwenye
sikio lako
Ø Kama
sikio lako ni kituo basi wewe ni Absalomu wa sasa.
Ø Unaonaje
ukimkuta mtu anamsema baba yako au mama yako mzazi je utafurahia ? Mchungaji
wako ni mzazi wako wa kiroho. Mithali
30:17.
vi.
Toa maelekezo mazuri wakati wa
dharula. Kwa mfano anapochelewa.
Ø Mtu
anayeambatana anamtetea kiongozi wake kwa gharama yoyote ile 1Samweli 18:1- 3 Wewe ni wathamani kuliko watu elfu kumi mlinde kiongozi kwa uwezo wako wote.
vii.
Inapotokea kwamba mchungaji wako ameshindwa kufika
kwenye sherehe au popote wajulishe kwamba alikuwa anapenda kuwepo lakini kuna
jambo lisilozuilika limemfanya asije.
viii.
Kama wewe ni mzee kiongozi siku
zote wakumbushe washirika kwamba wewe sio mchungaji ila ni mzee tu.
Yohana
3:28 “ Ninyi wenyewe mwanishuhudia kuwa nalisema mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake”
Yohana alipoulizwa wewe ndiwe
kristo akasema mimi siye “kama unasikia ugumu na hufurahi kuwaambia watu kuwa kuna mtu
aliye juu yangu ambaye ndiye baba yangu, ujue unayoshida au tatizo.
ix.
Kiongozi, msaidizi aliyeambatana
vizuri huwaambia washirika wanaomshukuru kuwa nayeye amejifunza kutoka mahali
fulani.Yesu aliwaambia watu kuwa ukimwona mwana umemwona baba.
Yohana
5:19 “ mwana hawezi kutenda neno mwenyewe
ila lile ambalo amwona baba anatenda kwa maana yote ayatendayo yeye ndiyo
ayatendayo mwana vilevile”
x.
Unapohudumia popote ni vizuri
washirika wajue kuwa unafanya kwa niaba ya kiongozi wako wala si kwa niaba yako
mwenyewe.
xi.
Tunaposema kwa jina la Yesu hiyo
hufanya watu waone kuwa tunafanya kwa niaba ya Yesu na hii humpa heshima Yesu. Furahi
kabisa kutoka ndani unapoona mchungaji wako anainuliwa
Yohana
3:30 “Basi hii furaha yangu imetimia yeye
hanabudi kuzidi bali mimi kupungua”
xii.
Hakikisha kuwa kila kitu
kinaendelea vizuri kwa mchungaji wako.Anapendwa,anaheshimiwa na yuko salama.
xiii.
Ufurahi ukiona kiongozi wako
ameingia mahali, iwe sherehe au msiba.
Kama
haufurahi ujue roho ya uasi inaanza
kukutafuna taratibu.
xiv.
Mheshimu mke au mme wa mchungaji,
mtumikie au kama unazawadi mpe.
Mtu
anaempokea mke au mme wa mchungaji amempokea mchungaji na anaemdharau
amemdharau mchungaji.
xv.
Uwe na muda wa
kuongea na mchungaji wako, ni muda wa kujifunza.
Jifunze
kitu kutoka kwake siku zote.
Ø Usione
tabu kuwa karibu na mchungaji, jifunze vitu vipya.
xvi.
Chukua mafundisho ya mchungaji
wako kama yako. Mfano kanda, vitabu, CD/DVD
xvii.
Kwenye mahubiri yako usiache kumnukuru
kiongozi wako kama mmoja wa watu waliofanikiwa kihuduma.
xviii.
Tendea kazi maamuzi na mipango
yake.
Wazo lake zuri lakini……………….
xix.
Usianzishe ushirika bila ruhusa.
xx.
Kumpa mchungaji zawadi. “Mithali
18:16”
xxi.
Kumsindikiza na kumpokea
mchungaji anaposafiri.
xxii.
Wakati wa ushauri ni vizuri kujifunza
kumsaidia sawasawa. Usichangie ushauri kinyume na aliotoa mchungaji.
Ø Usijaribu
kuleta hekima nyingine yoyote.
Ø Wewe
msaidie kiongozi kwa kusisitiza anachosema.
a)
Umeelewa anachosema mchungaji ?
b)
Unaelewa anachokusaidia mchungaji
?
c)
Mchungaji anasema haya kwa sababu
anakupenda.s
d)
Natamani kipindi kile nilichokuwa
kwenye hali kama hii, ningepata mtu wa kunitia moyo hivi.
xxiii.
Kiongozi anaeambatana huandika
yale mchungaji anasema na kufundisha.
a) Kuandika
ni hali ya unyenyekevu.
b) Kutoandika
ni hali ya uasi.
xxiv.
Anaeambatana yuko tayari kumtetea
kiongozi wake kutokana na makosa yanayoweza kujitokeza katika shughuli za kila
siku.
Ø Hakuna
asiyekosea.
Ø Sasa
ole wako ukosee halafu una watu wasioambatana na wewe.
xxv.
Kutoa ushauri mzuri kwa mchungaji na
ukikataliwa hachukii.
xxvi.
Anaeambatana anatosheka na nafasi anayopewa.
Ø Upako
maradufu wa Elisha (2 Samweli 2:1-14)
Ø Tahadhari
(Warumi 16:17) waangalieni.
SURA
YA NNE
MBINU ZA KUWALETA WATU KWA YESU.
Tunaweza kutumia mazingira katika kuhubiri na
kufundisha Neno la Mungu. Yesu alitumia mazingira katika kuhubiri Injili.
Alisimulia habari zilizoendana na utamaduni wa watu kwa kutumia vitu vya
kawaida vilivyopatikana katika mazingira yao.
Alitumia mifano ya ngano, mtini, zabibu,
kondoo, mnara , uvuvi na vitu vingine vingi
katika kufundisha kweli za
kiroho.
Mazingira yalikuwa ni uwanja ambapo wanafunzi
wa Yesu walifanyia kazi kweli
walizojifunza.
Katika kipengere hiki tutaangalia vitu viwili
Yesu alivyotumia katika kufundisha ambavyo ni Uvuvi wa samaki na ukulima yaani
udongo.
1.
UVUVI WA WATU.
Mstari wa ufungo.
“Yesu
akawaambia, njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu”. Marko 1:17
Wakati Yesu alipoanza huduma yake
ya hadharani hapa duniani aliwaita watu
kadhaa ili kuwa wanafunzi wake wa awali.
Agizo(amri) lake la kwanza
lilikuwa ni kujizidisha kiroho. Kama wangemfuata, yeye angewafanya wavuvi wa watu.Wangeanza kuvua kiroho wanawake na wanaume kama wao.
Ujumbe wa mwisho wa Yesu kwa
wanafunzi wake ulikuwa ni wito kwa uzazi
na mazidisho ya kiroho.
“Lakini
mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika Uyahudi
wote na Samaria na hata mwisho wa nchi. Akiisha kusema
hayo;walipokuwa wakitazama akainuliwa
wingu likampkea kutoka machoni pao”
Matendo ya Mitume 1:8-9
Ni jinsi gani wanafunzi wangeweza kutimiza hili
agizo kuu walilopewa na Yesu?
Namna gani kundi hili la watu wangejizidisha na
kuufikia ulimwengu wote ?
a. Mbinu za mazidisho.
Yesu alifunua mbinu maalumu
ambazo zingewawezesha wanafunzi wake kutimiza agizo kuu. “Kuzaa Kiroho” Mojawapo na muhimu ya mbinu hizi zilitolewa kama
sehemu ya Agizo kuu katika Matendo ya Mtume 1:8.
Wanafunzi
wangejizidisha kupitia kuvikwa nguvu na
Roho Mtakatifu.Mbinu
zingine zilifunuliwa pale wanafunzi walipoanza kujizidisha na kuufikia
ulimwengu kwa Injili. Mbinu hizi
zimeandikwa katika kitabu cha Matendo ya mitume. Na nyaraka katika Agano jipya.
Mada inalenga kutoa ufafanuzi wa
hizi mbinu za mazidisho. Somo hili linakufundisha wewe jinsi ya kutumia
mbinu hizi ili kuweza kujizidisha kiroho na kuweza kutimiza Agizo kuu la Mungu.
Lakini kabla ya yote unapaswa
kuelewa maana ya kujizidisha.
Kuzidisha
ni
kuongezeka mara nyingi kiidadi kwa kujizidisha.Kitu kinapojizidisha huzaa zaidi
na zaidi katika ufanano uleule.Mazidisho ni matokeo ya kuzidisha.
Mfano 3×3 = 9, wakati 3+3
=6. 4×3 maana yake ni kwamba namba 4 zinatakiwa kuwa tatu, yaani 4, 4, 4
ambako huleta jawabu la 12. Hivyo kuzidisha huleta jawabu kubwa kuliko
kuongeza. Jambo la msingi hapa ni kwamba namba moja hujirudia mara kadhaa katika mfanano ule.
Katika ulimwengu wa asili
wanawake na wanaume wanazaliana wenyewe kwa
kuwa na watoto. Wanajizidisha kimwili.
Mazidisho
ya kiroho yanatokana na kuzaliana kiroho. Mwamini huzaa kiroho kwa
kuwashirikisha Injili watu wengine
wasiomjua Mungu (wasiookoka) kwa kushuhudia
na kuhubiri na kuwaongoza hao aliowashuhudia au kuwahubiri kuwa waamini na
kuwawezesha kuwa wanafunzi wa Yesu.
Biblia inadhihirisha mbinu za ki
Mungu kwaajili ya mazidisho ya kiroho.
Mbinu
ni
mpango uliowekwa kwajili ya kufanikisha lengo fulani mahususi. Au ni hatua
zinazowezesha jambo fulani kufanyika kwa ufanisi kama ilivyokusudiwa.
.
Lengo
halibadilikji. Tunatakiwa kuzaa kiroho na kuufikia ulimwengu
wote kwa Injili ya Yesu Kristo. Kuna mbinu mbalimbali ambazo kwazo lengo hili
laweza kifikiwa . Mbinu hizi kwa pamoja
huitwa methodolojia ya mazidisho.
Wakati Mwamini anafanyia kazi mbinu za ki Mungu za mazidisho matokeo
yake huwa ni uzao wa kiroho.Yaani
waamini wapya huzaliwa kiroho katika mji wa mimba ambao ni kanisa.
b. Wito kwa matendo
Watu ambao Yesu aliwaita kwanza kuwa wanafunzi wake walikuwa ni wavuvi.Walikuwa ni watu wenye
kazi. Hawakukamata samaki kwa
wakati mmoja. Walitumia nguvu kubwa kuvua na kupata samaki wengi wa kila aina.
Wakati Yesu alipowaita kuwa
wavuvi wa watu alidhihirisha mpango
wenye kufanana na ile kazi yao ya
uvuvi kwaajili ya mazidisho ya
kiroho. Wanafunzi wake walitakiwa kuvua
watu toka kila taifa, tamaduni, lugha na makabila yote. Nyavu zao za kiroho
zingejazwa.
Yesu aliwaita watu kwaajili ya kazi .Alisema angewafanya kuwa wavuvi wa
watu.Hawangekuwa watazamaji tu katika mpango wa Mungu.Wangekuwa washiriki
wakuu kwa kuwa wavuvi wa roho
za watu.Wito wa Yesu bado ni sawa.
Haujabadilika.Tunapaswa kuwa wavuvi wa watu. Kama si wavuvi basi si wanafunzi.
c. Wavuvi wa watu
Kwanini Yesu alitumia mfano wa
uvuvi kuwaita wanafunzi wake ?
Kwanza ulikuwa ni
mfano ambao wangeuelewa kwa urahisi.Hawa
watu waliishi kwa shughuli ya uvuvi.
Kazi ya uvuvi ilikuwa ni kitu ambacho walitumia nguvu zao nyingi na muda wao
mwingi. Wakati Yesu alipowaita kuwa wavuvi walielewa kwamba wangewavua samaki (watu) katika ulimwengu wa kiroho.
Walielewa pia mahitaji ya wito huo. Uvuvi wa kiroho ungehitaji kujitoa
kikamilifu. Kutoa muda na nguvu.
Pili
Yesu
alitumia mfano wa uvuvi kuwaita wanafunzi wake kwa sababu kuna kanuni za uvuvi wa asili zinazoweza kutumika katika uvuvi wa watu (uvuvi wa kiroho).
Baadhi ya kanuni hizo ni:
1.
Unapaswa kwenda
mahali samaki walipo.Kama
unataka kupata samaki unapaswa kwenda samaki walipo. Samaki huishi majini. Huwezi kuwapata samaki kwa kuwasubiri ukiwa
juu ya mlima au ukiwa jangwani. Mvuvi wa
watu unapaswa kwenda mahali ambako watu ambao hawajaokoka wanapatikana au
kuishi. Watu ambao hawajaokoka
wanapatikana katikia maeneo mbalimblai huwezi kuwasubiri katika mejengo ya
kanisa ndipo uwavue. Nenda mahali
wanakopatikana, mfano
sokoni,mashuleni, hospitalini, magerezani,maofisini majumbani na mahali pengine
popote wanakopatikana na kisha wavue
2.
Lazima uchunguze mazingira. Katika uvuvi wa asili mvuvi anapovua
huzingatia mazingira, huchunguza kina cha maji, aina ya maji, ili kujua kama ni
maji ya chunvi au la, namna upepo unavyopiga. Mambo haya yote kwa kawaida hutoa
tathimini ya aina ya mtego na mbinu unazopaswa
kutumia Kuvua. Hizi pia ni mbinu utakazotumia katika
uvuvi wa watu. Kweli hizo hapo juu ni
sawa kabisa katika mambo ya kiroho.
Nilazima uchunguze mazingira
ambamo watu wanaishi. Nini mahitaji yao? (Tambua mahitaji yao) Nini kinaendelea katika maisha yao? Hii itakusaidia wewe kujua mbinu utakazotumia katika kuwavua watu hawa.
Yesu alipokutana na mwanamke
kisimani katika Injili ya Yohana 4 alichunguza mazingira
aliyomkuta yule mwanamke . Alikuwa anatafuta maji ya kawaida. Yesu alitumia hitaji hili la mwanamke kumsaidia kutambua hitaji lake la kiroho.
Mbinu aliyotumia ilimleta mwanamke
katika ufalme wa Mungu.
Kama huchunguzi mazingira katika uvuvi wa kiroho (watu) utajikuta mwenyewe unavua
juu ya mlima. Kwa sababu hujui watu
wanakopatikana na jinsi ya kuwafikia.
3 .Tumia mbinu mbalimbali. Mvuvi bora
hutumia mbinu mbalimbali katika kuwakamata
samaki. Hutumia vitu mbalimbali
ili kuwavutia samaki. Hutumia zana mbalimbali za uvuvi . Aina mbalimbali za
samaki huvutiwa na mbinu mbalimbali za uvuvi.
Ndiyo maana mvuvi bora hutumia mbinu mbalimbali. Mvuvi aweza kujifunza
baadhi ya mbinu hizo katika vitabu
vinavyohusu uvuvi. Anajifunza mbinu zingine kutokana na uzoefu na uchunguzi wa kina.
Mbinu anazotumia hubadilika lakini lengo daima linabaki kuwa lilelile. Kukamata samaki.
Kama unataka kuwa mvuvi bora wa watu
unapaswa kutumia mbinu mbalimbali. Watu wanatofautiana hivyo hata vitu
vinavyowavutia vinatofautiana. Wengine
huvutiwa na mahubiri au mafundisho aukufarijiwa wakati wa matatizo. n.k. Mbinu
za uvuvi wa kiroho zinatofautiana lakini lengo daima ni lilelile. Kupata roho zilizopotea na kuzileta kwa
Yesu Kristo.
4.
Unapaswa kutoa nje na kurudisha tena. Haijalishi mbinu unayotumia, unapswa
kuitupa nyavu majini na kuitoa tena.
Katika uvuvi wa kawaida jinsi
unavyotega mitego yako majini ni jambo muhimu sana. Unatakiwa kutega mitego
yako kwa umakini sana . Pia unapaswa kuwa makini katika kuwatoa samaki kwenye
mitego baada ya kuwakamata.
Katika ulimwengu wa roho tumeahidiwa
kwamba tukilitoa Neno la Mungu halitaturudia bure. Litafanikisha lengo katika maisha ya watu Isaya 55:11.
Unapotumia Neno la Mungu utakuwa katika
shabaha kila wakati na hatimae litawakamata wanawake na wanaume nakuwaleta
katika ufame wa Mungu.
5.
Tambua majira na nyakati.Majira ma
nyakati huathiri sana shughuli ya uvuvi katika ulimwengu wa asili.
Baadhi ya samaki huhama na hawawezi kupatikana katika baadhi ya kanda wakati wa
majira fulani. Samaki wakubwa hukamatwa
mapema mchana wanapokuja katika eneo la juu la uso wa maji ili kupata
chakula. Kama utavua katika majira
yasiyo sahihi au muda usio sahihi huwezi kuwakamata samaki wengi. Wakati ni muhimu sana katika uvuvi wa
kiroho pia.
6.
Lazima uwe mvumilivu.Katika
ulimwengu wa asili mvuvi hutakiwa kuwa mvumilivu. Ni lazima asubiri samaki
waingie kwenye mtego aliotega na kukamatwa.
Hii pia ni kweli katika ulimwengu wa roho.
“Kwahiyo
ndugu vumilieni hata kuja kwake Bwana. Tazama mkulima hungoja mazao yake ya
nchi yaliyoyathamani, huvumilia kwaajili
yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho” Yakobo 5:7.
C.
Kuzaa kiroho
Katika ulimwengu wa asili samaki
hupelekea kutokea kwa samaki wengine wengi kwa njia ya kuzaliana. Uvuvi katika
ulimwengu wa asili husababisha mazidisho ya samaki .
Uvuvi katika ulimwengu wa roho husababisha mazidisho ya watu katika ufalme wa Mungu. Uzazi wa
kawaida husabisha mazidisho ya watu walio hai. Uzazi wa kiroho husababisha pia mazidisho ya watu walio hai kiroho.
Hii haiji kutokana na programu za kibinadamu. Uzazi wa kiroho huja
kupitia mtiririko wa maisha ya kiroho
toka kwa Mungu. Katika maisha ya kawaida ya binadamu maisha ya kiumbe
kipya huanza katika tumbo la uzazi la mwanamke(uterus) na
seli hai moja . Seli hiyo hujizidisha
hadi mtu kamili anapokuwa amefanyika.
kisha mtoto huzaliwa.
Uzazi wa kiroho pia ni sawa na huo.Huanza na mtiririko wamaisha ya ki-Mungu kwa mtu mmoja , hujizidisha
katika tumbo la kiroho la uzazi ambalo
ni kanisa nakisha mtoto wa kiroho huzaliwa.
2.
UDONGO.
Andiko: Mathayo 13:3-9, 18-23
Yesu alitoa
mifano mingi iliyohusu kilimo. alizungumzia
habari za mpanzi, habari ya wakulima. N.k
Kutambua udongo wa kiroho wenye mbolea.
Katika ulimwengu wa kawaida wakulima huchunguza udongo kwanza kabla ya kupanda
mazao yao kwa sababu kuu tatu ambazo ni :-
Sababu
ya kwanza:- Wanataka kuchagua udongo bora kabisa ambako wataelekeza nguvu
zao zote. Wanajua kwamba udongo wenye mbolea
ya kutosha ndio utakao leta mazao
mengi.
Sababu ya pili: Kutambua
udongo duni ili waweze kujua namna ya
kuuandaa kwa kilimo. Waweze kutambua namna udongo huo unavyoweza kuboreshwa na
kufaa kwa kilimo.
Sababu ya tatu: Kutambua
udongo ili kujua mbinu zinazotakiwa
kutumika katika kilimo.
Kutambua
kwamba kama itahitaji kutumia kilimo cha umwagiliaji, aina ya mazao
yanayotakiwa kupandwa na namna ya uvunaji mazao.
Utafiti wa
mazngira katika ulimwengu wa roho
unafanana na kile wakulima wanachofanya katika
ulimwengu huu. Tunawachunguza,
watu, na maeneo kwa sababu tatu ambazo
ni:-
i.
Tunataka kujua eneo lenye mbolea zaidi kiroho.
Baadhi ya maeneo yako tayari kwa mavuno ya
kiroho. Biblia inasema kwamba watendakazi ni wachache katika uwanja wa mavuno,
hivyo tunataka kujikita katika maeneo
ambayo yako tayari kwa uvunaji.Lengo letu kuu ni kutoa kipaumbele kkwa maeneo
yaliyo tayari kwa mavuno.
ii.
Kutambua mbinu tunazoweza kutumia
kufanya ili eneo lisilofaa liweze kufaa kwa mavuno ya kiroho. Kuna baadhi ya
maeneo ambayo hayako tayari kuipokea Injili, Maeneo hayo ni sawa na udongo usio
na rutuba yanahitaji mikakati maalumu ili yaweze kufaa kwa mavuno ya kiroho.
iii.
Ili kutambua mbinu nzuri zaidi za
kiuinjilisti na umisheni zenye kuleta matokeo makubwa katika kuwaleta watu kwa mwokozi.